TCU YATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameitaka 
Bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU),kuhakikisha wanawezesha vyuo kufanya udahili na kuhakikisha elimu inayotolewa Vyuoni iwe bora pamoja na Ufaulu mzuri lengo likiwa ni kutengeneza Taifa lenye watu wasomi wanaokidhi vigezo.

Pia Prof. Mkenda  ameitaka Bodi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na kutenda haki katika kutekeleza majukumu yao na sio kutumika vibaya na badala yake ichape kazi.

Waziri huyo ameyasema hayo leo Januari 19,2023 Jijini Dodoma wakati akizindua Bodi hiyo amesema TCU inatakiwa  kuwezesha utambuzi wa vyuo vikuu vya nje ya nchi na kwenda kufanya uchunguzi kuhusu ubora na nafasi ya vyuo hivyo  ili kuwasaidia vijana wa kitanzania wanapokwenda kusoma nje wasome katika vyuo bora na vyenye ushindani.

Amefafanua kuwa TCU ina kazi kubwa ya kuwezesha na kudhibiti  ubora hivyo itumie nafasi hiyo kuifungua nchi katika sekta ya Elimu ndani na nje ya nchi.

"Chapeni kazi msimuangalie mtu usoni na kuzingatia Sheria, kufanya kwa haki kwani Bodi yenu ina kazi kubwa mbili ya kwanza kuwezesha na pili ni kudhibiti, sasa kazi ya kudhibiti ina lawama sana na lazima mkubaliane nazo,"amesema.

Kawa upande wake Mwenyekiti wa Tume hiyo Prof.Penina Mlama amemhakikishia Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyowaagiza likiwamo la  kuifungua nchi kimataifa kwa kuwapeleka wanafunzi wengi kusoma Vyuo vya nje ya nchi.

Amesema kuwa agizo hilo litazaa matunda Kwa kuongezeka kwa kasi ya Udahil,kusimamia ubora wa elimu inayotolewa na kuhakikisha vyuo vikuu vinasimama imara kuhimili na kuyamudu mabadiliko yanayotokea dunian

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU