INSPEKTA CLAUDIA AIANGUKIA CCM KUTHIBITI VITENDO VYA UKATILI MKURANGA


 Na mwandishi wetu,Pwani

MKUU  wa Dawati la jinsia Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Inspector Claudia Dominick Mselle amewaomba Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Mkuranga washiriki katika mapambano ya kuthibiti vitendo vya ukatili katika Wilaya hiyo Ili kumaliza kabisa tatizo la vitendo vya ukatili vilivyokithili wilayani humo.

Ombi hilo ameliwasilisha katika Mkutano wa Halmashauri kuu maalumu ya CCM iliyofanyika wilayani Mkuranga ambapo Mkuu huyo wa Dawati la jinsia Wilayani humo alipata nafasi ya kutoa mada.


Amesema wilayani humo kumekuwa na kuripotiwa kwa matukio ya vitendo vya ukatili wa kingono, ukatili wa kimwili.

Amesema viongozi wote watoe ushirikiano katika mapambano ya kuthibiti vitendo vya ukatili kwa watoto na Wanawake wilayani humo.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA