WANAFUNZI 80 TIA WAPATIWA ELIMU YA BRELA


Na Mwandishi wetu Dar es salaam 

Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),  wametoa mafunzo kwa wanafunzi 80 wa chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Taasisi kuhakikisha kuwa elimu  kuhusu urasimishaji wa Biashara inawafikia wadau mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo yametolewa  chuoni hapo Machi 25, 2023 Kurasini, jijini Dar es Salaam kwa wanafunzi wanaosoma Fani ya Usimamizi wa Biashara (Business Administration). 

Wanafunzi hao  wamewapatiwa  elimu kuhusu taratibu za  usajili wa kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, utoaji wa Hataza pamoja utoaji wa Leseni za Biashara Kundi "A"  na Viwanda.

Pia  wameelekezwa kwa  vitendo jinsi ya kutuma maombi mbalimbali kupitia Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).

Afisa Sheria wa BRELA Bw. Lupakisyo Mwambinga akiwasilisha mada kuhusu utaratibu wa  Usajili wa Kampuni na Majina ya Biashara ameeleza kuwa urasimishaji wa biashara unawezesha kupata fursa mbalimbali na kupanua wigo wa kibiashara. 

Kwa upande wa  Msaidizi wa Usajili wa BRELA, Bw. Abdulkarim Nzori ameeleza  jinsi Miliki Ubunifu inavyoweza kuwanufaisha wabunifu mbalimbali, kwakuwa ubunifu wowote unaanza na binadamu, hivyo ni vyema wakasajili bunifu zao ili kuwanufaisha wao na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA