Na Asha Mwakyonde, Dodoma
JESHI la Wananchi la Tanzania (JWTZ),limetangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kwa vijana wa kitanzania ambao wamemaliza mkataba wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea katika jeshi la kujenga taifa (JKT) na kurudishwa majumbani wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne hadi shahada ya uzamili.
Pia Jeshi hilo limewataka Watanzania
kutokurubuniwa kwani hakuna njia ya mkato katika kupata nafasi hizo bali zaidi vigezo vilivyowekwa na sifa za kupata nafasi hiyo,
Akizungumza jijini Dodoma Machi 09,2023 wakati akitoa taarifa hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Habari na uhusiao wa JWTZ, Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema see sifa za waombaji ni vijana
wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 26 kwa wenye elimu ya kidato cha 4 na cha sita na umri usiozidi miaka 27 kwa wenye elimu ya juu.
Luteni Kanali Ilonda, ameeleza vigezo vitakavyozingatiwa wakati wa katika maombi hayo kuwa mwombaji awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa mwenye kitambulisho cha Taifa,awe na afya nzuri na akili timamu,awe na cheti halisi cha kuzaliwa,vyeti vya shule nav yeti vya taaluma.
"Nafasi hizi zinawahusu wale ambao tayari wamemaliza mikataba yao ya mafunzo ya miaka miwili na kurudishwa majumbani na wenye vigezo vilivyotajwa vya kuomba nafasi hii," amesema Luteni Kanali Ilonda.
Ameongeza kuwa vigezo vingine kijana awe hajatumikia Jeshi la Polisi,magereza,Chuo cha Mafunzo au Kikosi maalumu cha kuzuia magendo na asiwe ameoa au kuolewa.
Utaratibu wa jinsi ya kutuma maombi Luteni Kanali Ilonda ,ameeleza kuwa maombi yote yaandikwe kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi hilo Dodoma kwanzia leo Machi 9 hadi Machi 20 ,Machi 2023 yakiwa na viambatanisho kama vya nakala ya kitambulisho cha taifa au namba ya nida,nakala ya cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule na chuo,nakala cheti cha JKT na namba ya simu ya mkononi ya muombaji na maombi yanaweza kutumwa Kupitia njia ya barua pepe ulinzimagazine@tpdf.mil.tz
0 Comments