Na Sifa Lubasi Kondoa
MWENYEKITI wa Wanawake Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Dodoma Fatuma Mshui amewataka wanawake kuwa wabunifu ili kuleta mabadiliko katika matumizi ya teknolojia kwani ni nyenzo muhimu itakayowawezesha kukuza biashara zao.
Alisema hayo juzi wakati wa mahojiano kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.
Álisema kuwa matumizi ya teknolojia ni nyezo muhimu katika kuchochea.usawa. wa kijinsia ambao pia unachochewa na mabadiko ya teknolojia
"Kuna umuhimu mkubwa kwa wanawake kuwa wabunifu katika maisha ya kila siku katika kujifunza mabadiliko ya teknolojia, iii kukuza biashara zao" alisema.
Mshui alisema kuwa teknolojia imekuws na manufaa makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo biashara
'Watu wengi wamekuwa wapata mafanikio zaidi kutokana na matumizi ya teknolojia katika kuwaongezea kipato ndio maana ubunifiu na mabadiliko ya teknolojiani muhimi," Álisema.
"Sisi kama wanawake tumejitokeza sana Ili kumpa sapoti Rais Samia kwa kuwa anafanya kazi kubwa sana na kazi anaiweza, kama wanawake tupo nyuma yake kutoa sapoti , Rais Samia anaupiga mwingi, lazima tumuunge mkono kwani sisi ni Jeshi kubwa" alisema
Alisema juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita zinatakiwa kuungwa mkono na wananchi wote.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA wilaya ya Kongwa , Sophia Boma alisema kuwa katiika kufanikisha usawa wa kijinsia kuna unuhimu mkubwa kwa wanawake kujifunza mambo mbalimbali kwa ajili ya ustawi wa shughuli zao za kila siku ikiwemo namna bora ya kufanya biashara
Kaulimbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya wanawake ni ‘Ubunifu na teknolojia kwa usawa wa kijinsia.’
Wakati wa maadhimisho hayo Mkuu wa wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema dhamira kuu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ni kutoa fursa kwa jamii kupima utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya maendeleo na uwezeshaji wa wanawake wote duniani.
"Lengo kuu la kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ni kutoa fursa kwa jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za kikanda na kimataifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na uwezeshaji wanawake.
0 Comments