Na.Elimu ya Afya kwa Umma
Katika kukabiliana na Ugonjwa wa Surua Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na Timu za Uendeshaji wa huduma za Afya ngazi ya Mikoa (RHMT ) na Halmashauri (CHMT ), Katika Mkoa wa Tabora zimeanza kutoa Elimu kuhusu umuhimu wa chanjo kwa Watoto wenye Umri kuanzia miezi 9 hadi miaka 5 ili kuweza kuwakinga na maambukizi ya mlipuko wa ugonjwa wa Surua.
Elimu hiyo imetolewa katika Kata mbalimbali zilizopo Tabora mjini na Kata tatu zilizopo nje ya mji ambazo ni ,Ndevelwa ,Ifucha ,na Itonjanda ambapo lengo la zoezi hilo ni kuwafikia wananchi katika maeneo yao na kuwapa Elimu kwa kutumia magari maalumu ya kufanyia matangazo (PA).
Utolewaji wa Elimu hiyo kwa kutumia magari hayo utawafanya wananchi wa Mkoa wa Tabora kupata mwamko wa kupeleka watoto kupata Chanjo na hivyo kuwakinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Surua.
0 Comments