Na Asha Mwakyonde Dodoma
WAWEKEZAJI wameshauriwa kuwekeza kwenye mashamba ya zabibu kwa kujenga hoteli za kisasa na nyumba za kulala wageni ili kuwavutia watu kwenda kuona mashamba hayo na kupata mvinyo ikiwa ni kufanya utalii wa ndani.
Pia Watanzania wametakiwa kujiwekea malengo ya kuweka akiba kidogo kidogo kwa ajili ya kwenda kutembelea hifadhi za wanyama pampoja na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.
Hayo yamesemwa Jijini Dodoma Machi 13,2023 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi Jeshi la Uhifadhi Ofisi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), kiunganishi cha hifadhi hiyo Dodoma Noelia Myonga amesema wanaendelea kutoa elimu kuhamasisha jamii utalii wa ndani.
Amesema kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amewaonesha njia katika Royal Tour aliyoifanya mwaka jana ambapo wanavisemea vivutio vyao na kwamba katika utafiti mdogo walioufanya wameona kuna changamoto ya utalii wa ndani kwa jamii.
"Tunatarajia ifikapo mwaka 2025 kupata watalii milioni 5 kutoka nchi nzima kwa sasa tuweze kuweka makundi maalumu ya wenye uhitaji," amesema Dk. Myonga.
Dk. Myonga ameongeza kuwa wanahifadhi kwa ajili ya watu kwenda kuwatazama wanyama mbalimbali na kufurahia ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla huku akitolea mfano wenye hoteli.
0 Comments