WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KUFIKISHWA MAHAKAMANI


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

SERIKALI imejipanga kuchukua hatua za kisheria kwa wale ambao watakaidi kulipa deni la msingi la malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi watafikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na 
kubadilisha hati ya umiliki ili zirejeshwe kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na kugawiwa kwa watu wengine.

Pia wamiliki wa vipande vya ardhi wametakiwa kuchangamkia fursa ya muda wa nyongeza ulioongezwa
wa kulipa deni la msingi la kodi ya pango la ardhi kwa kuwa  Aprili 30 mwaka huu ndio mwisho.

Akizingumza jijini Dodoma Aprili 12,2023 Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Denis Masami amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alitoa msamaha wa riba ya malimbikizo
kwa wamiliki wote wa vipande vya ardhi ambao walitakiwa kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba hiyo na kwamba awamu ya kwanza ya msamaha huo ulianza Julai hadi Disemba mwaka jana .

Mkuu huyo wa kitengo ameeleza Kuwa 
Kipindi cha nyongeza kilichotolewa na Rais cha kulipa deni la msingi la kodi ya pango la ardhi kimebakia siku chache.

" Mtakumbuka Rais Dk. Samia alitoa msamaha wa riba ya malimbikizo kwa wamiliki wote wa vipande vya ardhi ambao walitakiwa kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba hii, awamu ya kwanza ya msamaha huu ulianza Julai hadi Disemba mwaka jana katika kipindi hicho cha miezi sita wamiliki 6000 waliojitokeza kuchangamkia fursa hii iloyotolewa," amesema. 

Masami ameongeza kuwa baada ya kipindi hicho wananchi wengi waliiomba serikali kuona namna ya kuweza kuongeza muda ambapo iliongeza miezi miwili kuanzia Machi hadi Aprili mwaka huu.

Amesema hadi sasa wananchi waliochangamkia fursa ya msamaha  ni 8725 na deni la msingi lililolipwa ni zaidi ya bilioni 31.5 na kwamba riba itakayosamehewa ni bilioni 21.3 huku akisema  wananchi wengi wamepata nafuu ya msamaha huo iliyotolewa na Rais Dk. Samia.

Masami amewataka wananchi kujitokeza kuchangamkia fursa ya kulipa deni la msingi katika kipindi hicho cha mwisho na kwamba baada ya muda huo wa nyongeza.

Amesema matarajio yao ni wamiliki wote ambao wanadaiwa kuchangamkia fursa hiyo na kwamba  zaidi ya wananchi 200,000 hadi 300,000 hawajajitokeza kuilipa kodi ya pango la ardhi huku akieleza wapo wanaolipa kidogo kidogo na kuwaomba kukamilisha ndani ya kipindi cha msaamaha.


Naye Kamishna wa Ardhi  Msaidizi Mkoa wa Dodoma Jabir Singano amesema katika Mkoa huo kwa kipindi cha awamu zote hizo jumla ya wananchi 1200 wameweza kuchangamkia fursa hiyo na kufanikiwa  kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.2

Amesema kuwa jitihada nyingine walizozifanya ni kukwamua miamala 50  ya maombi ya umilikishaji ambayo ilikwama , kotroo namba 201 zilitolewa kwa ajili ya kuongeza makusanyo ambapo ni makusanyo ya kodi ya pango la ardhi na mengine yanayotokana na umilikishaji pamoja na huduma nyingine wanazozitoa.

"Kimsingi tunawaasa wananchi kutumia nafasi hii ili kulipa deni la misingi la pango la ardhi katika kipindi kilichobaki kufikia Aprili 30 mwaka huu," ameeleza Singano.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA