BRELA YAWAPIGA MSASA WAHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA BUGANDO


 Mwanza

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA imetoa mafunzo katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Mwambata cha Bugando jijini Mwanza, ili kuongeza uelewa kuhusu Miliki Ubunifu.

Akizungumza katika Mafunzo hayo Mei 8, 2023 katika Chuo  hicho,  Afisa Mwandamizi  kutoka BRELA Bw. Raphael Mtalima amesema Bunifu mbalimbali zikitumiwa zinaweza kutatua changamoto ikiwemo za Afya katika jamii na kuwakuza kiuchumi wabunifu na wafanyabiashara.

Katika mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na  wahadhiri na watumishi wa kada mbalimbali  wa Chuo hicho  wameelekezwa namna wanavyoweza tumia bunifu zao kutatua changamoto za Afya na Sayansi  ya Tiba ili kujikwamua kiuchumi na kutengeneza ajira kwa watu wengine.

Wakufunzi hao pia wamepata  fursa ya kukumbushwa kuwa Miliki Ubunifu ni mali kama mali nyingine japo haishikiki na wala haionekani, inayotokana na mtu kutumia akili kubuni vitu mbalimbali, hivyo wabunifu na wafanyabiashara wanayo nafasi kutumia bunifu zao kama vile Hataza, Alama za Biashara na Huduma zilizosajiliwa BRELA  kutambulisha bidhaa au huduma wanazitoa na wanaweza kuziuza au kuzikodisha  alama hizo pale inapobidi hivyo kunufaika na bunifu zao.

Maafisa wa BRELA  wanaendelea na zoezi la kutoa Mafunzo katika Vyuo Vikuu mbalimbali vilivyopo jijini Mwanza, ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Tanzania cha Mtakatifu Agustino (SAUT),Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) pamoja na Vyuo  vya Mafunzo ya ufundi stadi (VETA)  na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU