DK.GWAJIMA: WAZAZI WANALINDA MALI ZAO KULIKO WATOTO


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma 

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima amesema wazazi wamekuwa wepesi wa kulinda nyumba, shamba mifugo lakini hawawalindi watoto jambo linalosababisha watoto hao kufanyiwa vitendo vya ukatili vya kulawitiwa bila wao kujua na hawaoni thamani ya kumlinda mtoto.

Pia amewataka wazazi kukaa vikao kutathimini suala la maadili na upendo wao pindi wanapotofauyiana ili kuepuka athari kwa watoto ambao wengi wanazikimbia familia zao baada ya kupona wazazi hao wakigombana mbele yao.

Akizungumza Jijini Dodoma  Mei 15,2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya familia iliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere squre jijini hapa Dk. Gwajima ameeleza kuwa hofu ya Mungu imeondoka wazazi wakipotelewa na mbuzi kutwa kwa balozi lakini watoto wapo mitaani mzazi haoni shida.

Amesema takwimu za vitendo vya ukatili hasa kwa watoto zinaonesha asilimia 60 ukatili unafanyika nyumbani huku akiwataka wazazi kujenga tabia ya kuwalinda watoto wa dhidi ya vitendo vya vya ukatili.

"Mbuzi akiibiwa kwa mjumbe hakukaliki lakini watoto wetu hatuwalindi matokeo yake unakuta mtoto kafanyiwa vitendo vya ulawiti sisi hatuna hata habari hii inaonesha wazi hawaoni thamani ya watoto isipokuwa mali ndio zinalindwa," amesema Dk. Gwajima.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amezindua kampeni ya Kitaifa lengo likiwa ni kuhakikisha maadili yanalindwa na kuendana na mila na desturi za nchi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Fatma Toufiq amesema kuwapo kwa maadili na upendo familia hazitakuwa na watoto wa mitaani huku akisema ni wajibu wa kila familia kuwa na upendo na kwamba baba au mama ana wajibu wa kulinda familia yake.

"Tukiwa na malezi na mafunzo bora tutakuwa na familia bora na hakutakuwa na watoto wa mitaani lakini tukikengeuka tutakuwa na familia zisizo na upendo na maadili," amesema.

Naye  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.John Jingu ametoa wito kwa jamii kuitumia siku hiyo na  kutafakari  namna gani familia zinatimiza jukumu la malezi na ustawi wake huku akisema ni Azimio la kimataifa lililofikiwa mwaka 1993 kupitia baraza la Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Mrakibu msaidizi wa Polisi Dk. Ezekieli Kyogo, amesema kuwa kama familia zitakuwa sawa mzigo wa matukio ya uhalifu yatapungua nchini.

Ameongeza kuwa uwepo wamatukio ya kiuhalifu yanasababishwa na watoto ambao hawajalelewa katika familia yenye maadili ikiwamo wazazi kutoelewana.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI