Na Asha Mwakyonde,Dodoma
WAHITIMU wa Klabu ya Maadili ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
wametakiwa kwenda kuzingatia walichojifunza na kuwa raia wema waendako ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi wa maadili.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma Mei 14,2023 katika mahafali ya tatu ya Klabu hiyo na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi za Taaluma kutoka chuo hicho Dk.Yohana Mgale wakati akimwakilisha Mkuu wa Chuo hicho Profesa Hozen Mayaya amesema Chuo hicho kina wanafunzi takribani 10,400 na wengi wao ni vijana hivyo kuwepo kwa Klabu hiyo itawasaidia vijana hao kuwa na maadili bora.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wao kama Chuo wanatambua vilabu mbalimbali vya wanafunzi ilivyopi chuoni hapo kikiwemo cha maadili na kwamba wanajua maadili ndio msingi wa maendeleo katika jamii hivyo Klabu ya Maadili ni muhimu katika Chuo hicho.
Ameongeza kuwa Klabu hiyo imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za Chuo na imekuwa ni chachu kubwa kuwasaidia vijana hao kuwa maadili bora katika nyanja mbalimbali na kwamba wataendelea kuweka mazingira wezeshi ili vilabu hivyo viendelee kuwepi chuoni hapo.
"Tunawapongeza vijana wote ambao wamehitimu tunaamini wataendelea kuwa raia wema, mabalozi wema wa Chuo chetu , tunaamini kwamba elimu waliyoipata kupitia Klabu hii itaenda kuwasaidia katika maisha yao ya baadae," amesema.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
na Masoko kutoka chuo hicho Godrick Ngolly ambaye pia ni Mlezi wa Klabu hiyo amesema chuo hicho kimetengeneza mazingira rafiki na wezeshi kwa ajili ya wanafuanzi hao kujishighulisha katika maeneo mbalimbali ikiwamo kushiriki kwenye vilabu
"Shukrani pekee kwa uongozi wa chuo kwa kupafanya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kuwa sehemu ambayo vijana wanapata fursa ya kuonesha uwezo wao, vipaji ,vipawa vyao kwenye maneno mbalimbali yakiwamo katika uongozi," ameeleza Ngolly.
Amefafanua kuwa Klabu ya Maadili ilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na lengo la kuwafanya vijana wajitambue kutokana na ulimwangu wa sasa hususani jamii ya kitanzania inahitaji vijana wenye maadili hivyo wanajukumu la kueneza suala la maadili katika ngazi mbalimbali.
Kwa upande wake Afisa Maadili Sekretarieti ya Maadili, Joshua Mwambande amesema wanafunzi hao waliohitimu maadili wanatia matumaini kwa kuwa wamekuwa wakijifunza na kutamani kujua maadili ya viongozi wa Umma.
Ameeleza kuwa vijana hao wameonesha wapo tayari kuitumia elimu ya maadili huko wanaponda katika jamii na hata Vyuo vingine.
"Tunangalia uwezekana wa kuendelea kuwa na mahusiano nao hata baada ya kumaliza masoma yao kuanzia shule za msingi hadi Vyuo, tunaamini wahitimu hawa wataenda kuwa mabalozi wema katika maeneo watakayo kwenda kuishi," amesema.
Aidha amewataka wahitimu hao kuzingatia maadili na kufuata taratibu ,kanuni za mahali pa kazi na katika jami ambapo kwa sasa kuna mabadiliko mengi ambayo yanaathiri tamaduni za nchi.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo Mwaraba Ally amesema kuwa safari ya uongozi wao ilianza mwanzoni mwa mwaka jana ambapo walikuta chama kikiwa na wananchama 100 na hadi sasa wameongezeka na kufikia 245.
Ameongeza kuwa kama Klabu ya Maadili kuna mambo ambayo wameyafanya katika jamii yakiwamo kuchangia damu kwa wenye uhitaji, kutoa misaada kwa watoto yatima na kufanya usafi sehemu mbalimbali siku za Jumamosi pamoja na kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo chuoni hapo.
"Tunapozungumzia suala la maadili ni jambo pana kila jamii inatakiwa iishi kwa kufuata taratibu, misingi ya maadili kama Klabu tunatamani kuongeza idadi ya wananchama ili wanapohitimu waende na kuwa mabalozi kwenye jamii inayowazunguka,nawashauri ambao bado hawajajiunga wajiunge,"ameongeza.
Klabu hi ina manufaa makubwa inatujenga kimsingi, kiuelewa kiueledi kuanzia chuoni hapa hadi mitaani tunapoenda amesema Mwaraba.
Jovan John ni mhitimu aliyekuwa Afisa Uhusiano wa Klabu hiyo amesema kuwa elimu aliyoipata kupitia Klabu ya maadili ataenda kuelimisha vijana wenzake sehemu atakayoenda na kuwachukulia sheria kwa kufuata tarabibu pale inapohitajika kwa wanaokiuka maadili.
"Ninachojivuni kutoka Klabu hii hapa chuoni ni elimu niliyoipata kama silaha ya kwenda kuwa mwalimu wa wasiojua maadili katika jamii ninayoenda kukutana nayo," amesema.
Ameongeza kuwa kitu ambacho hawezi kukisahau katika Klabu hiyo ni ushirikiano wa wenzake huku akiwaasa wanaobaki kuendelea na ushirikiano huo chuoni hapo.
Naye Martha Mariseli ambaye pia ni mhitimu wa Klabu hiyo ameiomba serikali soma la maadili kutolewa vyuoni aliamini itawasaidia vijana kuwa na maadili na kujua mipaka yao kwa kuzingatia maadili hayo.
Ameeleza kuwa wamejifunza mengi na wataenda kuyatumia mafunzo hayo na kwamba Klabu imemfunza mambo mengi awali hakujua taratibu za uongozi zilivyo.
0 Comments