SERIKALI KUZIJENGA BARA BARA ZA NUNGWI KATIKA MAENEO YA UTALII


 Zanzibar 

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kuzijenga barabara zote zinazoenda katika maeneo ya utalii Nungwi na Kendwa kutokana na sekta hiyo kuchaingia sehemu kubwa katika uchumi wa Zanzibar.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ameeleza hayo wakati alipofanya ziara ya kuzikagua barabara mbali mbali zilizipo katika eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waziri Dk. Khalid amebainisha kuwa, Jumla ya Kilomita 12.5 za barabara zinazotoa huduma katika maeneo ya utalii zitajengwa katika eneo la Nungwi ili kuondoa changamoto inayowakabili wananchi na wawekezaji wa hoteli katika maeneo hayo.

Mara baada ya kuzikagua barabara hizo Mhe. Waziri amesema Serikali itaanza kuzijenga barabara zinazoendea katika hotel ya Zalu pamoja na barabara inayoendea katika eneo la uwanja wa ndege wa Nungwi kwa hatua ya awali.

Amesema Serikali itaanza na barabara hizo kutoka na urahisi wake huku Serikali ikiendelea kufanya uchunguzi kwa barabara zilizokuwepo katika maeneo ya makaazi ya wananchi ili kuona namna bora ya kuweza kuyaondosha maji kwa kujenga misingi ya kupititishia maji.

"Tumeamua kuanza na barabara zile mbili ambazo hazina changamoto, wataalamu wetu wanahitajika kufanya uchunguzi zaidi kwa barabara zinazopita katika makaazi  ya wananchi kwani pia zipo baadhi ya nyumba italazimika kuondoshwa kabisa ili kufanya utanuzi wa barabara" Alifafanua Mhe. Waziri

Aidha, Mhe. Waziri ameeleza tayari Mhe. Rais ameshatoa maelekezo ya kujengwa barabara zote zinazokwenda katika maeneo ya utalii katika kiwango bora kwa kuziwekea misingi ya kupitishia maji.

Wakati huo huo Mhe. Waziri  amefika Kibele Mkoa wa Kusini Unguja ili kujionea vifaa vitakavyotumiwa na Kampuni ya URKUN kujenga barabara mbali mbali ikiwemo barabara ya Jumbi - Tunguu, barabara ya Charawe- Ukongoroni- Bwejuu.

Akiwa katika eneo hilo la Kibele Mhe. Waziri amejiridhisha juu ya uwepo wa Lami ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara hizo.


 

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI