Dar es salaam
WATUMISHI wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa katika muda uliobaki kufikia mwisho wa mwaka 2022/2023.
Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw.Godfrey Nyaisa, amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza watumishi hodari pamoja na watumishi wote, iliyofanyika Mei 12, 2023, katika ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam.
“Ndugu watumishi, hivi karibuni Wakala imefanikiwa kujijengea heshima na imani kwa serikali na wananchi kutokana na kutoa huduma bora, kwa haraka na kwa urahisi, kwa kutumia mifumo ya TEHAMA, hivyo kuwezesha kutimiza malengo yake kwa asilimia 100 au zaidi kila mwaka” amesema Bw. Nyaisa.
Aidha Bw.Nyaisa amesisitiza kwamba ni jambo muhimu kwa Wakala kuendelea kutunza heshima na imani hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwaelekeza Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo kuhakikisha kwamba malengo yote waliojipangia yanakamilika kwa muda uliopangwa.
Akitaja mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha mwaka 2022/2023 ambao unaelekea ukingoni, yametokana na mchango wa watumishi wote wa Wakala na kutaja baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezajii wa malengo hayo hadi kufikia Mei 9, 2023, kuwa Wakala imefanikiwa kukusanya kiasi cha TZS.Bilioni 25,237,269,777 kati ya lengo iliyojiwekea hadi kufikia mwezi Juni, 2023 la kukusanya shilingi bilioni 28,904,217,240, kiasi hicho cha fedha ni sawa na asilimia 87 ya lengo lililowekwa kwa mwaka.
Ameeleza.kuwa mafanikio hayo yanatokana na Wakala kusajili Makampuni 12,398 kati ya 13,100 sawa na asilimia 95, Majina ya Biashara 23,075 kati ya 25,000 sawa na asilimia 92, Hataza 53 kati 35 sawa na asilimia 151, kutoa Hataza 16 kati ya 35, sawa na asilimia 46, maombi ya Hataza yaliyowasilishwa kupitia ARIPO ni 212 kati ya 650 sawa na asilimia 33, Alama za Biashara na Huduma 3,272 kati ya 4,120 sawa na asilimia 79, kutoa Leseni za Viwanda 160 kati ya 200 sawa na asilimia 80, kutoa vyeti vya Usajili wa Viwanda 35 kati ya 44 sawa na asimia 80, kutoa Leseni za Biashara 13,327 kati ya 13,750 sawa na asilimia 97.
0 Comments