SERIKALI KUBORESHA MADAWATI YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA


 Na WMJJWM, DODOMA 

NAIBU Waziri ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kunakuwa na Mazingira rafiki yatakayowezesha Madawati ya Jinsia  kutoa huduma kwa weledi na ubora.

Mhe. Mwanaidi ameyasema hayo Bungeni Dodoma Mei 13, 2023 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum  Mhe. Zaitun Swai aliyeuliza mpango wa Serikali wa kuboresha mazingira ya kuhudumia na kulinda usiri wa madawati ya kijinsia kwa wahanga wa matukio  ya Ukatili wa kijinsia Nchini.

"Madawati mengi ya kupinga ukatili wa Kijinsia katika Vituo vya Polisi yalianzishwa kwa kutumia Majengo ya zamani ndani ya vituo vya Polisi.

Tunaendelea kushirikiana na wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia jeshi la Polisi ili kuboresha Madawati hayo, hata hivyo hadi sasa Madawati 79 yenye viwango yameshajengwa" amesema Mwanaidi 

Aidha, amebainisha kwamba Madawati ya Jinsia na watoto sasa yapo Vituo vyote vya  polisi nchini na yanaendelea kuundwa katika shule zote za Msingi na Sekondari pamoja na vyuo vyote ambapo hadi sasa Mabaraza ya watoto 560 yameshaanzishwa.

Katika Hatua Nyingine Naibu Waziri Mwanaidi amtumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Wabunge kuhusu sheria zinazo husika na Masuala ya Ubakaji na ulawiti  

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI