DK.GWAJIMA: SERIKALI IMEBORESHA HUDUMA ZA KIJAMII, IDADI YA WAZEE YAFIKIA ASILIMIA 8.1

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

IDADI ya wazee imeongezeka kutoka 2,507,568 hadi kufikia 5,008,339 ambayo ni sawa na asilimia 8.1 ya Watanzania 61,741,120 ni kutokana na kuboreshwa kwa huduma za kijamii nchini.

Pia Wakuu wa Mikoa wametakiwa kuhakikisha elimu ya kina inatolewa kwa wananchi juu ya haki, ulinzi, usalama na ustawi wa wazee.

Akizungumza jijini Dodoma Juni 7,2023
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, Mkoani Dodoma katika kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15, yenye Kaulimbiu isemayo  "Wazee Wanastahili Heshima na Usikivu Wetu”

Dk. Gwajima amesema katika kulinda haki ya wazee kuishi, pia Serikali imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji kwa Wazee.


Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki kuwashughulikia ipasavyo wale wote watakaobainika kufanya vitendo vya ukatili kwa makundi mbalimbali katika jamii hususani kwa wazee.

"Maadhimisho haya ni muhimu kwa ajili ya kuuhabarisha umma juu ya haki, ulinzi, maendeleo na ustawi wa wazee wetu hivyo Serikali imeendelea kuadhimisha siku hii ya kupinga Ukatili dhidi ya Wazee ambayo hufanyika kila  Juni Juni15," amesema Dk. Gwajima.

Aidha, waziri huyo ameisisitiza jamii kuacha kufanya ukatili kwa Wazee na makundi yote kwa ujumla huku akiwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimisha na kuendelea kukemea masuala ya ukatili nchini.

Maadhimisho hayo ya Kupinga ukatili Dhidi ya Wazee mwaka huu yatafanyika katika ngazi ya Mikoa kote nchini.

Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI