THBUB IMETOA MAPENDEKEZO KWA SERIKALI,JAMII KUHAKIKISHA TATIZO LA AJIRA KWA WATOTO LINATOKOMEZWA


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), iendelee kuhakikisha kuwa suala la kutokomeza tatizo la ajira kwa watoto linapewa kipaumbele katika utengenezaji wa sera, shughuli za kitaifa na kimataifa, katika ushirikiano wa maendeleo na katika mikataba ya kifedha, biashara na uwekezaji.

Pia jamii  imetakiwa kuendelea  kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu wote wanaowaajiri na kuwatumikisha ikiwa ni  pamoja  na Wazazi,walezi wahakikishe wanawatunza, kuwalinda na kuwapatia watoto mahitaji yao ya msingi.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma Juni 12,2023 na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mohamed Hamad
wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ajira kwa Watoto yenye  kauli mbiu  isemayo “Haki ya Jamii kwa Wote. Kukomesha Ajira ya Watoto!” amesema
serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iendelee kutoa elimu ya haki za mtoto na madhara ya ajira mbaya kwa watoto.

Ameeleza kuwa miongoni mwa sababu zinazoendelea kuchangia ajira kwa watoto ni pamoja na umasikini na jamii kukosa uelewa juu ya madhara ya ajira hizo, hali inayopelekea watoto kufanya kazi ngumu ili kujikimu.

 "Serikali na jamii  wahakikishe watoto wote wanahudhuria shule na hawawatumii kama vitega uchumi vya familia kwa kuwafanyisha kazi ngumu, zisizofaa na zinazowaathiri na iendelee kuhamasisha hatua za kimataifa kufikia haki ya kijamii na kuondoa ajira kwa watoto kama moja ya mambo yake muhimu;" amesema. 

Makamu huyo Mwenyekiti ameongeza kuwa Shirika la Kazi kupitia Mkataba wa Kimataifa Na. 138, liliweka umri wa ajira kuwa miaka 15 na kuendelea na katika Mkataba Na. 182 liliorodhesha ajira zisizokubalika kwa watoto na ambazo zinatakiwa kuzuiwa.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU