BRELA YANG'ARA YAPATA TUZO MSHINDI WA KWANZA MAONESHO YA SABA SABA 2023


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar uuhu Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhi tunzo ya mshindi wa kwanza katika kipengele cha Uwezeshaji wa Ukuzaji wa Biashara na Uwekezaji kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Andrew Mkapa wakati akifungua Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

WAKALA ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),imeibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza katika kipengele cha Uwezeshaji wa Ukuzaji wa Biashara na Uwekezaji kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," ambayo yamehitimishwa leo Julai 13,2023.

Katika kilele cha  maonesho hayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumza jijini Dar es salaam kwenye maonesho hayo katika banda la BRELA mara baada ya kutangazwa ushindi huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Andrew Mkapa ameeleza kuwa wameta tuzo tatu pamoja na Ile ya mshindi wa banda bora.

Kaimu Afisa huyo amefafanua kuwa tuzo ya kwanza ni kutoka kundi katika uwekezaji masuala ya uwekezaji na urahisishaji wa biashara, BRELA ni miongoni mwa wadhamini taasisi za serikali, wadhamini wa maonesho hayo ya biashara  na tuzo ya nne ni ya banda bora katika maonesho hayo.

"Nipo hapa kushirikiana nanyi katika mafanikio ambayo tumeyapata tuzo tatu, tuzo ya kwanza tulikuwa ni miongoni mwa wadhamini taasisi za serikali pia wadhamini wa maonesho haya ya biashara, vile vile tumepata tuzo nyingine ya ushindi wa nne wa banda bora katika mabanda bora ambayo yameshiriki maonesho haya," amesema Mkapa.

Aidha amewashukuru wafanyakazi wote wa BRELA huku akisema tuzo hizo zimepatikana kutokana na michango yao huku akiwataka kuendelea kujituma kutoa huduma kwa wateja wao ili kuyafikia mafanikio mengine zaidi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI