TANTRADE, ZEEF WAINGIA MAKUBALIANO NA MoU ILI KUENDELEZA WAJASIRIAMALI WA ZANZIBAR


Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam 

MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) wameingia mkataba wa makubaliano (MoU) na Wakala Wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEF),malengo yakiwa ni kuendeleza biashara na wajasiriamali wa Zanzibar.

Pia Wafanyabiashara wametakiwa kwenda Zanzibar kuwekeza na kujifunza zaidi juu ya mifumo ya kiteknolojia ili kupata fursa mbalimbali zilizopo

Akizungumza mara  baada ya kusaini mkataba huo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Ali Suleman Ameir
kwenye maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu SabaSaba, ameeleza uwa MoU itasaidia kukuza biashara na kufungua uwekezaji Zanzibar.

Amesema mkataba huo utawainua wajasiriamali wa Zanzibar na kwamba popote Tantrade itakapokuwepo  bidhaa za wajasiriamali hao  zitakuwepo

"Hii ni fursa kwetu na wajasiriamali  wataongeza ubora wa bidhaa ili tuweze kujitangaza kimataifa maonyesho hayo ni sehemu ya kudumisha undugu uliopo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar,” amesema Ameir.

Ameongeza kuwa katika siku ya Zanzibar  inatoa nafasi ya kutangaza bidhaa za Zanzibar, kutangaza utamaduni na kutangaza fursa zitokanazo na uchumi wa bluu .” Ameelza Naibu Waziri Ameir

Ameongeza kuwa Wakala Wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi imeweka miundombinu mizuri ya uwekezaji ikiwemo kuimarisha maeneo ya uwekezaji na upatikanaji wa huduma wezeshi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Latifa Khamis amesema wametenga siku maalum kwaajili ya Zanzibar katika maonesho hayo ili kujifunza utamaduni wa Zanzibar na kuangalia fursa zinazopatikana visiwani humo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU