Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam
VYUO vya City college of Health, Ilala Campus, Kilimanjaro Institute of Health Goba na Arusha vimeingia makubaliano na baadhi ya benki kutoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana wanamaliza kozi ya diploma lengo likiwa ni kuwaandaa katika kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri ajira serikalini au katika taasisi.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Julai 11,2023 Mtendaji Mkuu wa Vyuo vya City college Nuran Mwasha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema kuwa wanafuanzi wao wana nafasi kubwa ya kupata mitaji baada ya kumaliza Vyuo hivyo.
Mtendaji huyo ameeleza kubwa mwanafunzi atakapomaliza atajiendeleza kwa kujiari baada ya kupatiwa mkopo na kwamba vyuo hivyo vina mahusiano mazuri na Global Education Link ambao wanasafasirisha wanafunzi kwenda kusoma nje ya nchi.
Amesema kuwa wana ofa mbalimbali ambazo wanazitoa katika kipindi hiki cha msimu wa Saba Saba ikiwa ni punguzo la ada la aslimia 20 kwa wanafuanzi watakaojisajili kipindi hiki pamoja na chakula cha mchana bure.
" Tupo Saba Saba kwa ajili ya kuonesha huduma na bidhaa zetu na mara baada ya maonesho haya tunatarajia kushiriki maonesho ya nane nane ," amesema Mwasha.
Naye Afisa Udahili Coletha Sospeter amesema kuwa ada ni nafuu na kwamba inalipwa kwa awamu nne ndani ya mwaka mmoja na mwanafunzi atakae kaa bwenini hatalipia gharama ya malazi kwa kipindi chote cha miaka mitatu.
"Tunapenda kuwakaribisha wanafunzi wote ambao hakuweza kupata nafasi ya usajili dirisha la awali, tunawakaribisha nafasi zipo kwa kozi za, Clinical Medicines, Pharmaceutical science na social works," amesema.
Amewataka wanafunzi kuwahi katika awamu ya usajili ili waweze kupata nafasi za kujiunga na Chuo hicho ambacho kina ada nafaa na ofa ya saba ambapo italipwa 600,000 mwanafunzi anapoanza na baadae kidogo kidogo.
Kwa upande wake mmoja wa mzazi wa wanafunzi wanaosoma katika moja ya vyuo hivyo alipotembelea banda hilo Anna Kimaro amesema kuwa amevutiwa na ada ya yake ambayo ni nafuu na inalipwa kwa awamu nnee na kwamba uongozi una mvumilia mtu anapokwama.
"Mimi ni mzazi mtoto wangu anasoma Kilimanjaro Institute of Health nawashukuru walimu wanafundisha vizuri nilivyompeleka mwanangu alikuwa hataki kusoma kabisa kwa sasa amevutiwa kusoma pale.
Ameongeza amesikia ofa ya msimu wa saba saba kuhusu kupunguzo la ada hivyo amefika katika banda hilo ili kujiridhisha na kufanya maamuzi ya kumpeleka mtoto wa dada yake kusoma.
0 Comments