DCEA: SERIKALI KUFANYA UTAFITI MAENEO YANAYOLIMWA BANGI

Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam 

MAMLAKA ya kudhiti na kupambana na madawa ya kulevya Tanzania (DCEA), imesema serikali inampango wa kufanya utafiti wa maeneo yanapolimwa bangi na mirungi ili kubadilisha kilimo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima hao kulima kilimo mbadala kitakachokua na tija na kuwanufaisha.

Pia wazazi wameshauriwa kuwaleta watoto kwenye maadili mema na kuwapa elimu juu ya athari zinazotokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Kauli hiyo ya serikali ongezeko kubwa la matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo bangi na mirungi nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam  Julai 6, 2023  kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," Kamishna wa mamlaka hiyo Jenerali Aretas Lymo ameeleza uwepo wao katika maonyesho hayo ni  fursa kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya.

Kamishna huyo amesema serikali ina mpango wa kuhukikisha inatokomeza  dawa za kulevya zinaisha nchini kwa kuwawezesha watumiaji na walimaji wa dawa hizo ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo ili kuwakwamua kiuchumi.

"Mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na  Halmashahuri kwa vijana ina lengo  la kuhakikisha vijana hao wajiendeleza  na shughuli za kuwaingizia kipato hali itakayowasababishia kukosa muda wa kujiingiza katika makundi yasiyofaa," amesema.

Kamishna Lymo amesema kuwa kundi kubwa linaloingia  kwenye madawa ya kulevya ni wanafunzi na watoto ambao wapo mtaani hivyo mamlaka hiyo inatoa elimu na kuanzisha vilabu vya madawa za kulevya katika shule na vyuo ili kujenga uelewa kwa wanafunzi kuhusu athari za matumizi ya madawa ya kulevya.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA