Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam
WATANZANIA wamesisitizwa kutumia teknolojia ya mtandao (Internet), kupitia simu janja za kufanya usajili wa kupata
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ili kurahisisha ujajili huo kwa baadhi ya maelezo ya fomu ya maombi ya vitambulisho hivyo.
Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 5,2023 katika banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na msemaji wa mamlaka hiyo, Geoffrey Tengeneza kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema waombaji wakizaja fomu kupitia mtandaoni itabaki sehemu ndogo ya kwenda kukamilisha usajili huo katika ofisi za NIDA kama kupiga picha na alama za vidole.
Tengeneza amesema katika maonesho hayo banda hilo limeliwa likihudumia idadi kubwa ya watu siku hadi siku kadri maonesho yanayoendelea kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
Amesema huduma kubwa ambayo wanaitoa katika maonesho hayo ni kutoa fomu ya maombi pamoja na kuwaelekeza wananchi namna ya kujaza fomu hiyo.
Akizungumzia changamoto wanayokutana nayo maofisa wa mamlaka hiyo wakati wa kutoa huduma waombaji kutokukamilisha viambata vingine.
Amesema kuna makundi matatu yanavyosajiliwa kupata vitambulisho vya Taifa ambayo ni raia wa Tanzania, Wakaazi au wawekezaji pamoja na wakimbizi.
"Raia wa kigeni anahaki ya kusajili na kupata kitambulisho endapo atakuwa amekidhi vigezo vinavyotakiwa na kama ni raia wakimbizi lazima kuwe na kitu kinachomtambulisha ni mkimbizi na kama ni wawekezaji" ameeleza.
Amefafanua kuwa kuna raia wafanyakazi katika taasisi, mashirika ya kigeni wakiwa na kibali cha kufanya kazi nchini anasajiliwa kupata kitambulisho cha NIDA.
0 Comments