DK. YONAZI: SERIKALI IMEWEKEZA KATIKA TEKNOLOJIA YA KUKABILIANA NA MAJANGA

Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

SERIKALI imesema  kwa mwaka huu wa fedha imejipanga kwa ajili ya kuendelea kujenga uwezo kwa kushirikiana na wadau wa nje na ndani ya nchi ili kuhakikisha kwamba uwezo wake wa kukabiliana na majanga ya aina mbalimbali yakiwamo moto, majanga ya asili kama matetemeko na mafuriko unaboreshwa.

Serikali imewekeza katika teknolojia ambapo kwa sasa ina mifumo ambayo itusaidia kurahisisha kukabiliana na majanga ikiwamo kutoa viashiria vya awali kuratibu namna ambavyo wale ambao wanaowajibika kwenda katika eneo la tukio wanavyowezeshwa kwenda.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai  06, 2023 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dk. Jim Yonazi, alipotembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,"amesema  serikali  itaendelea kuelimisha jamii juu ya namna ya kukabiliana na kujikinga na maafa mbalimbali yanayotokea katika jamii.


Katibu hiyo ameeleza Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu ina jukumu la kuratibu namna itakavyo  itakabiliana na majanga katika nchi.

"Tupo hapa kutoa elimu, tunachofanya ni kuelimisha jinsi jamii  itakavyoweza  weza kujikinga na majanga mbalimbali
 ikiwemo ya asili kama milipuko ya Volkano, matetemeko na hata yale ambayo yanatokea katika mazingira ya kazi.

Aidha ameongeza kuwa serikali imeendelea kushirikiana na wadau katika kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa na kujiandaa, kukabiliana na majanga  yanapotokea.


Dk.Yonazi amesema majanga hayo yamekuwa yakileta madhara nchini na  kuathiri uchumi wa nchi  wa mtu mmoja mmoja na kwamba wizara imeendelea kuratibu namna bora kujenga uwezo wa utayari wa kukabiliana na majanga hayo.

Akizungumzia mfumo huo wa teknolojia amesema wanachi wanaweza kutoa taarifa hivyo serikali ina mifumo ya kitehama ambayo inatusaidia.

Dk.Yonazi ameeleza kuwa serikali ina mpango wa kuwa na uwezo wa kutanua uwezo wake wa kukabiliana na majanga nje ya nchi ili iweze kukuza uchumi na diplomasia na nchi jirani.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA