Na Asha Mwakyonde Dar es salaam
MANUFAA na matumizi ya mionzi katika karne ya sasa ni makubwa kwa kuwa mionzi inatumika katika sehemu mbalimbali kuhakisha usalama wa Watanzania unapatikana ikiwamo hospitalini inatumika katika matumizi ya X-ray,ultrasound na ST- SCAN.
Pia Watanzania wametakiwa kukitumia kituo cha nguvu ya Atomu kwa ajili ya kunufaika zaidi na bidhaa pamoja na utaalamu wa aina tofauti tofauti ambao wanaweza kuutumia katika maisha yao ya kila siku.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam Julai 7, 2023 na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga alipotembelea banda la Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC),katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema Tume hiyo inafanya kazi kubwa ya kuratibiwa, kuthibiti ili mionzi isiweze kuleta athari kwa wanaadamu.
Amesema kuwa mionzi ndiyo inayowezesha kufanya tafiti za namna mbalimbali ambazo zinawezesha kupata bidha, mbegu za aina nyingine zinazoweza kuwa ni bora zaidi na zinazoweza kupambana na mazingira ya tabia nchi.
Ameongeza kuwa wameweza kutumia tafiti hizo kwa ajili ya manufaa mbalimbali huku akisema wanafahamu wanamaeneo mengi katika Kanda mbalimbali na kwamba hawawezi kuagiza chakula kutoka nje, kutoa bila kuhakikisha kama kipo salama kwa upande wa mionzi na matumizi ya binadamu
"Tunafahamu ukienda Hospitali, ukitaka kupigwa X-ray na ultrasound, ST- ST- SCAN utatumia mionzi. Kazi inayofanywa na Tume hii ni kubwa bahati nzuri nimepata fursa ya kutembelea pale Arusha na kuona namna gani mionzi inaweza kuratibiwa, kuthibitiwa ili isiweze kuleta athari kwa wanaadamu," amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAEC ,Profesa. Lazaro Busagala amesema majukumu ya Tume hiyo ni kuhakikisha Watanzania wanakuwa salama wasijewakawa wanaathirika na hatari ambayo inaweza kusababishwa na mionzi.
Prof. Busagala ameongeza kuwa kazi kubwa wanaoifanya pamoja na kuhakikisha Watanzania wako salama wafanye biashara zao wakiwa salama huku akitolea mfano mfanyabiashara anaye peleka bidhaa za nje ya nchi zikiwa salama kwa matakwa ya kimataifa soko lake litaendelea kuwa salama kila inapoitwa Leo.
"Mfanyabiashara huyu ataendelea kujipatia kipato kampuni na biashara yake itaendelea kukua, tumefanya mabadiliko makubwa ndani ya miaka michache iliyopita mfano zamani mtu alikuwa anatumia kupata kibali kuanzia siku Saba hadi mwezi lakini kwa sasa ndani ya saa tatu anapata kibali chake cha kusafirisha mzigo wake hivyo tunamuokolea muda," ameeleza Mkurugenzi huyo.
Aidha Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wananchi kuitumia Tume hiyo na kwamba inaofisi zisizopungua 54 nchi nzima hivyo wananchi hao wanaweza kupata huduma karibu zaidi sehemu waliopo huku akitolea mfano wanaochimba kisima kama kunaweza kuwa na mamdini ambayo sio salama wakiitumia (TAEC), inaweza kuokoa maisha ya watumiaji wa maji hayo.
0 Comments