SERIKALI YAZINDUA INTANETI YA WAZI SABA SABA, UCSAF KUWEKA MTANDAO WA INTANETI MABASI YA DART


Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

WAZIRI Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnaye amezindua mtandao wa intaneti ya wazi
 (Free-Wifi), Julai 08,2023, katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,.

Pia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),kwa kushirikiana na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART),unatarajia kuweka mtandao wa intaneti ya wazi  katika mabasi yote ya mwendokasi.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mtandao huo, Waziri Nape amesema kuweka mtandao wa wazi sio uwekezaji mdogo umetumia gharama ya milioni 200 lengo ni kila mtanzania aweze kufurahia maisha.

Ameongeza kuwa huduma hiyo ambayo inapatikana katika maonesho sio jambo dogo ni fedha imewekwa makusudi ili kuhakikisha watu wanafurahia huku akiipongeza UCSAF kwa kazi kubwa wanaoifanya.

"Watu wengi wamepiga simu  wamefurahia kutumia huduma zenu niwahakikishie Watanzania ni maagizo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwamba tutawaunganisha katika maeneo yao ya shughuli zao popote kwenye masoko makubwa, maduka kama ulivyosema Mhandisi Albert Richard kwenye mabasi ya mwendokasi watu wapo wengi mtaweka niwapongeze kwa juhudi zenu," ameeleza Waziri Nape.

Ameongeza kuwa lengo la kuweka huduma hiyo ni kuhakikisha mtanzania popote alipo aweze kufanya kazi zake.

Awali akitoa maelezo mafupi kuhusu intaneti hiyo Mkurugenzi wa Uendashaji na Utafiti kutoka UCSAF, Mhandisi Albert Richard katika banda maalumu la kuzindua mfumo wa Intaneti hiyo amesema vituo 22 vya mtandao wa Intaneti vimefungwa katika maeneo 17 kwa gharama ya shilingi milioni 200.

Mhandisi Richard ameongeza kuwa mbali na Mradi huo tayari wamefunga katika maeneo mengine sita ambayo ni Dodoma Nyerere square, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Lungemba College Njombe, Buhongwa Mwanza, Tabora Market na Kiembe Samaki Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU