KAMPUNI YA TIGO YAPONGEZWA KWA KUTOA HUDUMA YA SIMU ZA MKOPO


Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam 

WAKAZI mbalimbali waliofika katika banda la Kampuni ya simu za mkononi Tigo wameipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma ya mkopo  wa kishua wa simu kwa kuzingatia hali halisi ya kipato cha Watanzania.

Wakizungumza jijini Dar es salaam walipotembelea banda la Tigo na kujipatia huduma ya simu za mkopo  katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," waliishukuri Kampuni hiyo kwa kuzingatia uwezo wa kila mtanzania na kutaka wamiliki simu janja.

Fatuma Abdallah ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es salaam amesema kuwa anejipatia simu ya mkononi kupitia huduma ya mkopo wa simu kutoka Kampuni ya Tigo.

"Nashukuru kwa huduma hii nzuri kwa sisi ambao wenye hali ya chini tunajipatia simu ya mkopo kwa kulipa kidogo kidogo kila siku, nawaomba Watanzania wenzangu waje wachukue simu hizi kulingana na hali zetu za kiuchumi" amesema.

Naye Mkazi wa Mbezi beach Alphonce Kilizi  amesema kuwa amechikua simu ya mkopo ya shilingi 90,000 ambapo atarejesha kila siku shilingi 1500 hadi atakapomaliza kuilipia.

" Unapewa simu kulingana na kiwango chako cha fedha zipo za bei tofauti tofauti kwa mfano mimi nimechukua simu ya shilingi 90,000 ni kutokana na kipato changu lakini zipo za bei ya chini na ya juu zaidi, " ameeleza.

Akizungumzia huduma hiyo Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Kanda ya Dar es salaam Robert Kasulwa  amesema lengo la kuweka huduma hiyo ni kila mtu aweze kumiliki simu janja na kwamba 
watu ni wengi wanaotembelea banda hilo na kufanya manunuzi ya simu kwa fedha taslimu na mkopo.

"Siku hii ya leo tunawakaribisha wateja wetu wanaokuja kwa ajili ya kununua simu lakini wengi zaidi ni wale wanaokuja kwa ajili ya mkopo wa kishua, tunawambia wateja wetu wanauwezo wa kumiliki simu janja za mkononi kwa bei rahisi ya kulipia kila siku kwa gharama ya kuanzia 1,000 na wanauwezo wa kulipia kupitia lipa namba," amesema.

Ameongeza kuwa wateja hao wakilipa kupitia namba hiyo wanaingia katika droo ya kujishindia fedha taslimu  kupitia kampeni ya 'Chawote' ambayo wanaweza kujishindia  dakika, ujumbe na kiasi cha shilingi milioni moja ambapo wanapata washindi zaidi ya 320 kwa siku.

Meneja huyo amewataka wananchi kutembelea banda hilo na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU