Na Asha Mwakyonde Dar es salaam
SERIKALi katika kufikia ujenzi wa kidigitali ni lazima kuwa na miundombinu inayosaidia uchumi wa kidigitali ikiwa ni pamoja na kutengeneza vibao vya anuani za makazi.
Pia ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa kidigitali ambao itawezesha kufikiwa kwa uchumi huo wa kidigitali.
Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 08,2023 Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika maonesho hayo ikiwa ni siku maalum ya TEHAMA iliyoandaliwa na kampuni ya TANZAKWAZA Kwa kushirkiana na Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), ili kufikia huko ni lazima sheria,sera na mikakati ifanane na mikakati ya kidigitali sawasawa na dunia inapokwenda.
Waziri huyo amesema kazi kubwa kwa serikali ni kuhakikisha mtandao uko salama uaminike na watu waweze kuutumia huku akiitaka Mamlaka ya Maendeleo Biashara na( Tantrade), kukutana na wadau kutoka Wizara yake kufanya tathmini kujua ni eneo gani la kuboresha kwa kuwa serikali inataka watu wa kidigitali kuteka maonesho hayo.
"Lazima kuwa na sera ya wabunifu Chipukizi (Status) katika eneo la digitali kwani walioko nchini wako vizuri na kuwepo kwa sera itasaidia kuondoa utapeli wa kimitandao," amesema Waziri Nape.
Aidha alisema katika uchumi wa kidigitali ipo haja ya minara ya mawasiliano kusambazwa nchini katika maeneo mbalimbali na kila wilaya iwe imeunganishwa na minara hiyo ya mawasiliano.
Ameongeza kuwa baadae wanataka wakuu wa wilaya wasitoke kwenye vituo vyao vya kazi kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya mikutano wataifanya wakiwa huko katika maeneo yaowakifanya kazi.
Waziri huyo ameeleza kuwa mifumo hiyo inaweza kusaidia hata kurahisisha uendeshaji wa kesi mahakamani hivyo hakuna ulazima kwa mshtakiwa kutoka mahabusu kwenda mahakamani bali taratibu zinaweza kuendelea,yakiwezekana hayo yote ni uchumi wa kidigitali ambao itasaidia kuondoa pia rushwa.
Pia ameita Tantrade kukutana na wadau kutoka Wizara yake na kufanya tathmini kujua ni eneo gani la kuboresha kwani serikali inataka watu wa kidigitali kuteka maonesho hayo.
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade,Latifa Khamis amesema huduma hiyo katika Maonesho hayo imerahisisha biashara kwa njia ya digitali ambapo ukataji tiketi umefanikiwa kwa asilimia 95,ugawaji wa sehemu za kufanyiwa biashara kufanikiwa kwa asilimia 99 ambapo waombaji wengi walituma maombi ya vitambulisho jambo lililopunguza msongamano.
Mkurugenzi wa TANZAKWANZA, Tumaini Magila amesema kampuni hiyo imeandaa majukwaa nane ya kimkakati kuhakikisha jamii inapata uelewa wa kutosha.
Akizungumza katika uzinduzi wa mtandao, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfumo wa Mawasiliano Kwa wote (UCSAF) Albert Richard alisema yapo maeneo 17 katika viwanja vya hivyo na zaidi ya sh mil 200 zinatumua kwa uwekezaji huo.
0 Comments