TMDA KUTOA MSAADA WA KIUFUNDI KWA WANAOANZISHA VIWANDA VYA VIFAA TIBA


Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam 

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),imejipanga katika kutoa msaada wa kiufundi kwa wanaotaka kuanzisha Viwanda vya bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi kuanzia kwenye mchoro ambao ni muhimu kwa kuwa unaonesha ramani nzima ya kiwanda kitakavyokuwa.

Akizungumza jijini Dar es salaam Julai 07,2023 Meneja  wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa TMDA Gaudensia Simwanza katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema msaada huo wa kiufundi una mchango mkubwa kwa yule anayetaka kuwekeza.

Meneja huyo ameeleza kuwa wanachokifanya serikali inamfuatilia na kumsaidia anayetaka kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda tofauti na kuanza ujenzi huo bila kutoa taarifa na kwamba madhara yake mwekezaji anaweza kubomolewa.

Amesema kwa upande wa kufuatilia ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa hizo wanaanzia tangu kwenye kiwanda na kwamba ukaguzi unaanza katika bidhaa zinapozalishiwa huku akisema mazingira ya uzalishaji yana mchango mkubwa katika kuhakikisha kile kinachozalishwa kina ubora na usalama.

"Tunatoa msaada wa kiufundi na kwa wale ambao wameshaanza kuzalisha tunaendelea kuwafuatilia milango ipo wazi mwekezaji anaweza kufika hatua fulani akaja tena kutuona TMDA kwenda kuangalia,"ameongeza.

 "TMDA inawapa miongozo unapotaka kuzalisha, kuangiza kitu fulani nini ufuate kufuata kabla ya kuanza uzalishaji mfano wenye viwanda malighafi zinazotumika katika vifaa  na zenyewe zitunzwe katika mazingira ambayo ni safi," ameeleza.

Ameongeza kuwa  hata wale wanaotaka kuangiza bidhaa hizo nchini nao wanapewa miongozo.

"Katika maonesho haya kitu ambaccho tuanenda nacho sambamba ni kauli mbiu yake kwetu sisi TMDA tunathibiti ubora,usalama pamoja na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi kikubwa ni kuwafikia wawekezaji mbalimbali wanaotoka nje na ndani ya nchi,"ameeleza.

Amesema kuwa lengo la ushiriki wao katika maonesho hayo ni kuwafikia na kuwaelekeza miongozo mbalimbali inayotolewa na Mamlaka hiyo kwa wawekezaji.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU