Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam
TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC),ina ofisi zisizopungua 52 nchi nzima lengo ni kuwarahisishia wananchi kupata huduma karibu zaidi na sehemu waliopo hasa wale wanaotoa huduma ya uchimbaji visima vya maji Ili kubaini madini ya Urani yaliyopo kwenye maji kama ni salama au la.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Julai 09,2023 Mkurugenzi Mkuu wa TAEC ,Profesa. Lazaro Busagala katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," amesema lengo la kufungua ofisi hizo ni kuhakikisha mwananchi anayechimba visima vya maji chini ya ardhi ambapo kuna madini ambayo hayajulikani kama Urani na kuanza kuyatumia maji hayo kabla kuyapima matokeo yake yanaweza kusababisha vifo vya watumiaji.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa kuwapo kwa ofisi hizo kunawarahisishia wananchi kupata huduma sehemu zaidi waliopo tofauti na awali walivyokuwa wakizifuata makao makuu.
"Tumefanya mabadiliko makubwa katika miaka hii michache iliyopita awali mtu alikuwa akitumia siku saba hadi mwezi kupata kibali cha kusafirisha mizigo ya biashara lakini kwa sasa vinatoka ndani ya siku tatu," amesema Prof. Busagala.
Prof.Busagala amewataka wananchi wahakikishe wanapata huduma zinazotolewa na TEAC ili, huduma, bidhaa wanazotumia zikiwamo za maji ya visima wanatumia yapo salama lengo likiwa ni kuepuka mionzi hatari.
0 Comments