T- PESA YAZINDUA HUDUMA YA AKAUNTI PEPE


Na Asha Mwakyonde Dar es salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Latifa Khamis, kupitia  T- Pesa amezindua Akaunti Pepe (Virtual Wallet ), ya  Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), ambayo itakayosaidia kuwarahisishia  watanzania kutumia huduma ya kifedha kupitia kiganjani mwako.

T -Pesa imeleta urahisi wa huduma za kifedha kwa watanzania na kumuwezesha mtu kupata huduma za kifedha kwa njia ya kidigitali hivyo ni hatua muhimu katika kukuza maendeleo ya digitali nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam  mara ya kuzindua huduma hiyo katika banda la TTCL lililopo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo amesema akaunti hiyo ni Teknolojia inayoruhusu watanzania hao kutuma na kupokea pesa kwa urahisi,kulipa bili, na kufanya manunuzi kwa njia ya kidijitali bila kuwa na SIMCARD.

Latifa ameeleza kuwa huduma hiyo imekuja wakati sahihi katika kipindi ambacho Serikali inasisitiza matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi.

"Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametilia mkazo sana juu ya matumizi ya teknolojia na kwa sasa tuanze kuelekea katika matumizi ya mifumo kwenda mbele," amesema.

Aidha ametoa wito kwa Shirika hilo  kuhakikisha huduma hiyo inakuwa  hadi kuwafikia waliopo vijijini  na sio mijini pekee.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa T-Pesa, Lulu Mkudde amesema Kampuni ya T-Pesa ni mdau mkubwa katika kukuza matumizi ya mifumo ya Kidigitali katika shughuli za kiuchumi na Kijamii.

"Uzinduzi wa akaunti pepe hii kupitia kauli mbiu ya "Kufungua milango kuelekea katika ujenzi wa taifa ya Tanzania ya kidigitali", dhamira ya Kampuni ya T-Pesa ni kuhakikisha inaendelea katika kuunga mkono Juhudi za serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa Tanzania ya Kidigitali ambayo kwa sasa imeanza kufanya kazi," ameeleza.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU