JKCI YAWASHAURI WATANZANIA KUPIMA MAGONJWA YA MOYO

Na Asha Mwakyonde,Dar es salaam 

WATANZANIA wameshuriwa kujitoke kwenda kupima afya zao kwa kuwa kupima mapema ni kujua afya na kupunguza kupata madhara ya magonjwa ya moyo na  kuzingatia kufanya mazoezi,kutokuvuta sigara ,kupunzuza unywaji pombe uliokithiri  kwani vitu hivyo vinachangia kupata magonjwa hayo na kuepuka unene uliokithiri.

Akizungumza Jijini Dar es salaam Julai 09,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dk. Peter Kisenge katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji," 
amesema wagonjwa wa moyo wanaongezeka wanaolazwa hospitalini ndio wanaoongoza hususan magonjwa ya Shinikizo la damu asilimia 25 ya magonjwa yote ya moyo ndio yanayoongoza.

Amefafanua kuwa sababu kubwa ya magonjwa hayo ni kwamba watu hawafanyi mazoezi na pia ni wavuvi kutembea muda mwingi wanatumia vyombo vya moto kama bajaji, pikipiki (bodaboda), hata kama safari sio za mbali.

"Nawashauri watu kufanya mazoezi, kutembea safari za karibu, kula vyakula vya lishe bora ambavyo havichangii unene pamoja na kuepuka kula vyakula vya sukari , wanga  kwa wingi hivi tujaribu kuviepuka tule vyakula vya mboga mboga na matunda, kuacha kuvuta sigara na kupunguza unywaji wa pombe tusizidishe chupa tatu hii itasaidia kupunguza magonjwa ya moyo," amesema.

Ameongeza kuwa magonjwa ya Moyo  yanazidi kuongezeka kwa kasi hivyo Taasisi hiyo inapokea wagonjwa wengi wa moyo zaidi ya nchi 20 za barani Afrika na katika maonesho hayo wanawaonesha watembeleaji  huduma hizo zinatolewa JKCI  huku akisema katika maonesho hayo  kuna nchi takribani 47 zimeshiriki. 

"Tumekuwa tukipata watu wengi kwenye banda letu kuja kupata huduma ya elimu ya tiba ya magonjwa ya moyo pamoja na watu kutoka nchi mbalimbali kuja kujionea huduma zetu," amesema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa katika maonesho hayo wameshiriki kwa ajili ya kuwapima wagonjwa, kuonesha huduma mbalimbali ambazo taasisi hiyo inazitoa za tiba ya moyo na upasuaji wake pamoja  na huduma ya tiba Utalii.

Taasisi ya Moyo ya JKCI imekuwa na uwekezaji mkubwa ambao serikali umewekwa kwa upande wa vifaa vya kutolea huduma za magonjwa hayo.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA