DUWASA:BILIONI 30.7 KUKAMILISHA MIRADI MINNE UCHIMBAJI VISIMA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

MAMLAKA  ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA),imesema kukamilika kwa miradi minne ya muda mfupi ya uchimbaji wa visima inayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 30.7 utaongeza upatikanaji wa huduma ya  maji kwa wakazi wa Dodoma.

Akizungumza jijini Dodoma leo Julai 28,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu utekelezaji na mwelekeo wa mamlaka hiyo  Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph amesema kukamilika kwa miradi hiyo itaongeza uzalishaji maji kutoka saa 13 hadi 19 kwa siku mwishoni mwa mwaka 2024 ambapo 
mahitaji ya sasa ni lita milioni 133.4 kwa siku huku uzalishaji ukiwa ni lita milioni 68.6.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa upungufu uliopo kwa sasa ni lita milioni 64.8 hali inayosababisha Mamlaka hiyo kuanzisha mipango ya muda mfupi, kati na mrefu lengo likiwa ni kutatua changamoto kwa wakazi hao.


Akizungumzia mkakati wa mamlaka hiyo amesema ni kuboresha Miundombinu ya Maji taka katika kata zote za Jiji la Dodoma na kuboresha upatikanaji wa maji mjini Dodoma na kuondosha majitaka kwa kushirikiana na Wizara ya Maji.

"Tunaendelea na utafiti, kuchimba na kuendeleza visima maeneo ya pembezoni mwa mji lengo la mpango huu ni kupunguza changamoto kwa wakazi katika maeneo haya," ameeleza Mhandisi huyo.

Ameongeza kuwa Mipango hiyo imegawanyika katika sehemu kuu zifuatazo, Muda mfupi, Muda wa Kati, Muda mrefu na Mpango wa Dharula/haraka Katika mpango wa muda mfupi.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI