NIRC: KUANZA UJENZI MABONDE 22, SKIMU MPYA 35


Na  Asha Mwakyonde, Dodoma 

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji. (NIRC),inatarajia kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye mabonde 22 yenye jumla ya hekta 306,361,  ambapo itaanza ujenzi  huo wa skimu mpya 35 zenye jumla ya hekta 111,390.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Julai 28,2023  Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Raymond Mndolwa Kuhusu utelezaji wa majukumu ya NIRC, amesema mbali na ujenzi huo ni pamoja na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji katika Skimu 24 zenye jumla ya hekta 32,092; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa mapya 100 yenye wastani wa mita za ujazo 936,535,700 na kuanza ujenzi wa mabwawa hayo.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa 
pia tume hiyo itajenga miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya pamoja (Block farms) yenye jumla ya hekta 79,518.46 katika Mikoa ya Kigoma, Njombe, Mbeya, Kagera na Dodoma kupitia programu ya Building Better Tomorrow (BBT).

Ameongeza kuwa ili kufikia malengo hayo Tume imepanga kutekeleza jumla ya miradi 822, ambapo miradi 114 ni ya ujenzi wa mabwawa na 103 ni ya ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji.

"Maeneo ya kipaumbele katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, kukamilisha ujenzi wa skimu mpya 25 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023, kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu 30 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023," ameeleza.

Amesema pia tume hiyo inatarajia kukamilisha ujenzi wa mabwawa 14 yenye mita za ujazo 131,535,000 yaliyoanza kujengwa Mwaka 2022/2023, kukamilisha usanifu wa mabonde 22 ya Umwagiliaji ulioanza Mwaka 2022/2023.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI