Na Asha Mwakyonde, Mbeya
BENKI ya CRDB imetoa mikopo yenye thamani ya trilioni 3.6 kwenye sekta ya Kilimo kwa kuwagusa wakulima 759,400
waliopo katika hatua ya uzalishaji wanaotoka kwenye vyama vya ushirika zaidi ya 472 nchi nzima.
Pia benki hiyo imewekeza mitaji yenye thamani ya Sh. bilioni 10.2
katika Benki za Ushirika (KCBL), iliyopo mkoani Kilimanjaro na benki ya TACOBA iliyopo Tandahimba, Mtwara lengo likiwa ni kuhakikisha inafufua vyama vya ushirika.
Hayo yamesemwa leo 2,2023 jijini Mbeya na Meneja Uhusiano upande wa Kilimo Biashara Ofisi za Kanda Mbeya, kutoka CRDB Gilbert Kyando kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula',amesema kuwa wameamua kumgusa mkulima wa kawaida.
Kyando ameongeza benki hiyo ndio benki pekee inayotoa mkopo yenye riba nafuu ya aslimia 9 kwenye sekta ya kilimo kwa kuwagusa wazalishaji ambao ndio wenye changamoto.
Amesema kuwa benki hiyo hadi kufikia Disemba 2022 ilikuwa imetoa mikopo yenye thamani ya trilioni 3.6 kwa wakulima na kwamba mikopo ambayo bado ipo katika vitabu vyao ni trilioni 1.2.
Amefafanua kuwa KCBL wamewekeza bilioni 7 na TACOBA bilioni 3.2 ili kuonesha benki za ushirika zinaweza kufanya kazi huku akisema pamoja na kuwekeza mitaji pia wamewekeza katika usimamizi na kujewangea uwezo wafanyakazi wa ushirika.
Meneja huyo amesema katika sekta ya kilimo benki ya CRDB imechangia asilimia 43 ya mikopo yote iliyopo kwenye sekta hiyo na kwamba wanahudumia zaidi ya benki 50.
Kyando amefafanua kuwa benki moja imetoa zaidi ya asilimia 43 huku akisema kwao ni mafanikio na kwamba wanakazi kubwa ya kuendelea kufanya.
"Mikopo mingi iliyotolewa imetolewa katika hatua za juu sio hatua ya uzalishaji ambapo benki nyingi zinaenda katika hatua za juu na kukimbia hatua za uzalishaji," ameeleza Kyando.
Amefafanua kundi lililopo katika hatua za juu ni mvuvi,mkulima na mfugaji huku akiwataka waliopo hatua za juu kwenye tabaka la uzalishaji.
Amesema watu hao hawakutani na changamoto za moja kwa moja zinazotokana na minyororo mbalimbali ya kilimo.
0 Comments