GCLA: DNA INAHUSIKA KWA WANAOTAKA MIRATHI


Na Asha mwakyonde, Mbeya

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA),imesema kuwa kipimo cha Vinasaba (DNA),kwa binadamu  ni kitu ambacho kinatumika ili kuweza kubaini mambo mbalimbali yakiwamo kujua ukoo.

Akizungumza jijini Mbeya leo 2, 2023, katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', 
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya, kutoka Mamlaka  hiyo ,Elias Mulima amesema kwenye mambo ya mirathi baba akifariki watonatokea watoto mbalimbali wanahitaji kupata urithi kwa aliyefariki.

Mulima amefafanua kuwa kesi inaenda mahakamani ambapo mahakama hiyo  inaamuru wahusika kufanya kipimo cha DNA kujua kama ni ndugu au mtoto wa baba aliyefariki.

"Kuna baadhi ya watu, watoto wanaibuka baada ya baba kufariki na kudai kuwa ni watoto wa familia hiyo, mtoto wa baba huyo aliyefariki hivyo DNA inatumika kwa kuchukua sampuli ya ndugu yaani baba mdogo au mkubwa kubaini kama kweli ni mtoto wa wa ukoo fulani," ameeleza.

Meneja huyo ameongeza kuwa kuna baadhi ya miili inaokotwa inakuwa haitambuliki ndugu zao ,mifupa hivyo kipimo cha DNA kinatumika ili kubaini ndugu husika.

Amesema wapo baadhi ya wanaume wanawatelekeza  watoto  na kukataa  kutoa huduma ya matunzo hivyo DNA inatumika kuthibitisha kwa kufanya vipimo ili kubaini watoto ni wao ili waweze kutoa huduma hiyo.

Mulima ameeleza kuwa Vinasaba hutumika katika majanga ya ajali za Majini, moto na kwamba miili inayotokana na majanga hayo haiwezi kutambuliwa kwa kutazamwa kwa macho hivyo wanatumia vinasaba ili waweze kubaini na kujua ndugu zao huku akitolea mfano ajali ya mafuta iliyotokea miaka ya nyuma mkoani Morogoro.

Amesema teknolojia ya upimaji wa vinasaba  imeweza kusaidia katika majanga mbalimbali yakiwamo ya moto,ajali za majini na  kutumika katika kutambua magonjwa mapema zaidi kabla haujaanza kuenea kama saratani na mengino huku akitolea mfano nchi za nje zinavyotumia Teknolojia hiyo  hugundua ugonjwa mapema.

Kwa mujibu wa Meneja huyo DNA pia inahusika kuwaachia huru ambao hawakuhusiki na matukutio ambayo yamewasababishia kukamatwa.

Akifafanua gharama za upimaji wa sampuli za vinasaba amesema kwa sampuli moja gharama yake ni shilingi laki moja (100,000).

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI