EWURA YAWAHAMASISHA WENYE MITAJI MIDOGO KUJENGA VITUO VYA MAFUTA

Na Asha Mwakyonde, Mbeya

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),inahamasisha ujenzi wa vituo vya mafuta vya gharama nafuu katika maeneo ya vijijini kwa walio na mitaji kuanzia milioni 40 hadi 60.

Akizungumza jijini hapa leo 2, 2023, katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', Afisa Uhusiano kutoka mamlaka hiyo ,Tobietha Makafu amesema wapo katika maonesho hayo kuwapatia wakulima na wananchi elimu ya namna ya wenye mitaji midogo watakavyoweza kufuata utaratibu wa kupata kibali cha ujenzi wa kituo pamoja na leseni.

Makafu amesema kuwa EWURA inafahamu wakulima wengi  wapo vijijini na wanatamani kufungua vituo vya mafuta hivyo katika maonesho hayo wanatoa elimu ya namna gani mkulima huyo anaweza kujenga kituo cha mafuta kwa mtaji mdogo.

"Tupo hapa kutoa elimu ya Udhibiti huduma za Nisha na maji, tumeileta elimu hii kwa wakulima pamoja na wananchi wanaotembelea maonesho haya, tunaamini mkulima ni mtumiaji mkubwa wa umeme maji pamoja na nishati ya mafuta ya petroli," amesema.


Ameongeza kuwa katika sekta ya Nishati ya umeme EWURA wanadhibiti na kutoa leseni kwa watoa huduma, kuweka viwango vya ubora pamoja na kupanga bei hivyo mkulima akifika kwenye banda hilo atajua ni kwa namna gani anaweza kupata huduma bora.

Makafu amesema katika sekta ya mafuta ya petroli wakulima wanatumia trekta kulimia, gari kusafirishia mazao yao watakapotembelea banda la EWURA watafahamu mamlaka hiyo inavyodhibiti ili waweze kupata bidhaa bora na kuzipangia bei.

Amefafanua kuwa EWURA ipo katika maonesho hayo kutoa elimu katika sekta ya Maji na usafi wa mazingira invyodhibiti, kumsaidia mtumiaji kujua matumizi bora ya maji hasa yanayotolewa na mamlaka za maji za mikoa, Wilaya pamoja na mijini midogo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI