TPHPA KUTOA ELIMU MATUMIZI SAHIHI, SALAMA YA VIUATILIFU NANE NANE MBEYA

 

Na Mwandishi wetu, Mbeya

MAMLAKA  ya Afya ya mimea na Uthibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA),imesema katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane),imejipanga kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu ,vinyunyizi,udhibiti wa visumbufu vya Mimea,taratibu za uingizaji wa mazao nchini na utoaji wa mazao nje ya nchi pamoja na usimamizi wa biashara ya viuatilifu (taratibu za usajili wa Viuatilifu na biashara za viatulifu.

Maonesho hayo  yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula', ambayo kitaifa yanaadhimishwa mkoni hapa kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Akizungumza Jijini Mbeya leo Agosti 2,2023katika banda la Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka hiyo Profesa Joseph Ndunguru amesema uwepo wao katika maonesho hayo lengo kuu ni kutoa elimu kwa wananchi wa mikoa ya Nyanda za juu kusini.


Mkurugenzi huyo  ameeleza kuwa Mamlaka hiyo inatoa elimu juu ya uhifadhi wa bioanuai za mimea, udhibiti wa visumbufu vya mimea kwa kutumia njia za kibaolojia, na udhibiti wa wa visumbufu vya mlipuko.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya maonesho ya hayo  2023 kwa upande wa Mamlaka hiyo Dkt Mujuni kabululu amewaomba wananchi kuendelea kutembelea banda hilo ambapo watapata fursa ya kukutana na wataalumu ambao watajibu maswali yote na kutoa elimu stahiki pamoja na kupokea changamoto mbali mbali za wakulima.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI