SHERIA YA SERIKALI MTANDAO INAVYOFANYIWA KAZI

𝗨𝘀𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗶𝘀𝗵𝘄𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗧𝗮𝗮𝘀𝗶𝘀𝗶 𝘇𝗮 𝗨𝗺𝗺𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝗱𝗮𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗵𝘂𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗩𝗶𝘄𝗮𝗻𝗴𝗼 𝗻𝗮 𝗠𝗶𝗼𝗻𝗴𝗼𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗦𝗲𝗿𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 𝗠𝘁𝗮𝗻𝗱𝗮𝗼.

DODOMA 

Maafisa wa  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kutoka katika taasisi mbalimbali za umma wameshiriki katika kikao kazi cha kuandaa na kuhuisha Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, ili kuhakikisha inaendana na Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019.  

Lengo ni kuhakikisha Serikali inakua na Serikali mtandao yenye tija na inayoongeza ufanisa katika utendaji kazi na utoaji huduma kwa Umma.


Kikao hicho kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), kilifanyika kwa siku 3 kuanzia Agosti 15, 2023 katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijijini Dodoma.

Viwango na Miongozo hiyo inapatikana katika Tovuti ya e-GA kupitia kiungo

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA