Na Asha Mwakyonde, Dodoma
JUMLA ya Vijana 3,258 wamenufaika na mafunzo katika Vituo vya veta vya Dodoma ,Manyara, Lindi,Singida Mikumi Gorowa na Dakawa kupitia programu ya kukuza ajira na ujuzi Kwa maendeleo Afrika(E4D), ulioanza kutekelezwa mwezi mei mwaka huu.
Hayo yameelezwa Jijini Dodoma leo 22, 2023 na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Abdalah Ngodu, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu Kongamano la ajira litakalofanyika tarehe 24 mwezi huu katika viwanja vya Nyerere square.
Amesema idadi ya Vijana hao wanatarajiwa kuwa nguvukazi yenye ujuzi kutokana na mradi huo na itatumika katika kukuza ajira kwenye miradi ya kimkakati ya uwekezaji kama bomba la mafuta na Bwawa la Nyerere.
Mkuu wa chuo cha ufundi cha Veta Dodoma Stanslaus Ntibara ,amesema hadi kufikia tarehe 19 mwezi huu jumla ya wanafunzi 1806 wa Mkoa wa Dodoma waliokuwa wameshahitimu mafunzo hayo.
Naye Mwakilishi Mshauri wa programu hiyo kutoka Shirika la GOPA, Leah Doto, amesema
mradi huo unalenga kuwaandaa vijana kupata ajira kwenye uwekezaji ambao unafanyika hapa nchini na kuweza kujiajiri
Tanzania ni Miongoni mwa nchi sita za Afrika zinazotekeleza mradi wa stadi za ajira Kwa maendeleo Afrika inayofadhiliwa na Wizara ya Shirikisho la Ujerumani la Ushirika la kiuchumi na maendeleo (MBZ) na Shirika la ushirikiano wa maendeleo la korea (KOICA).
0 Comments