WAHITIMU WA VETA KUPITIA MRADI WA E4D WAASWA


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WAHITIMU wa mafunzo ya ufundi kutoka vyuo vya  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),kupitia  programu ya kukuza ajira na ujuzi Kwa maendeleo Afrika(E4D), ulioanza kutekelezwa mwezi mei mwaka huu awametakiwa kuwa na ujasiri na kujiamini katika kutumia ujuzi wao.

Akizungumza leo Agosti 24,2023 jijini Dodoma Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde wakati akifungua kongamano la ujuzi na ajira  amesema uaminifu, uadilifu na bidii katika kazi ni vigezo muhimu katika mafanikio kwenye ajira ya kuajiriwa au kujiajiri. 

Waziri amesema Tanzania ina fursa nyingi za ujasiriamali na mahitaji makubwa katika soko la ajira. Kupitia mafunzo haya, vijana mmepata ujuzi unaohitajika katika sekta mbalimbali za viwanda, ujenzi, na teknolojia.

Amesema hiyo ni fursa nzuri ya kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kujenga ajira kwa wengine.

"Nendeni mkatumia ujuzi wenu vizuri na mkawe mabalozi wa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa kwenbye Vyuo vya VETA nchini," amesema.

Aidha ameqaomba waajiri, kuendelea kuwekeza kwa kuwatumuia vijana wenye ujuzi kuwapatia fursa za kazi na mafunzo ili waweze kuendeleza ujuzi wao na kuchangia katika ukuaji wa biashara zenu.

Ameongeza kwamba kuwekeza kwa vijana wenye ujuzi ni muhimui kwa kuwa nguvu kazi yenye tija na wanachangia katika kujenga jamii imara na taifa lenye maendeleo endelevu.

"Natoa wito kwa Wabia wa Maendeleo, na sekta binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa ajili ya kukuza ujuzi na ajira kwa vijana.Tunahitaji kuwekeza katika miundombinu bora ya elimu na mafunzo, kuboresha upatikanaji wa mitaji na mikopo kwa vijana wajasiriamali, na kuweka mazingira rafiki ya biashara,"ameeleza.

Naibu Waziri huyo amesema Vijana ni rasilimali muhimu na nguvu kazi yenye kuleta mabadiliko na kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu. 


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya VETA, CPA Anthony Kasore amesema mradi huu wa E4D amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imechukua jukumu kubwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na Ofisi ya Wazri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Shirikisho la Waariji nchini (ATE) pamoja na wadau wa maendeleo.

Amesema Mradi huo una lengo la kuongeza ujuzi wa vijana na kuwapa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira.

"Kongamano hili ambalo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Ujuzi na Ajira kwa Maendeleo ya Africa (E4D), linapewa umuhimu mkubwa katika kukuza ujuzi na kuimarisha fursa za ajira kwa vijana na wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi," amesema.

Amesema shabaha ni kuwafikia vijana 4,000 katika fani za Mechatronics, uchomeleaji viwandani, pamoja na ufundi bomba majumbani na viwandani.
CPA Kasore amesema tayari vijana 3,258 wamehitimu mafunzo hayo ambapo kwa upande wa chuo cha Chuo cha VETA Dodoma ni kufikia vijana 2200 na hadi sasa kimewafikia vijana 1,806.

Kwa upande wake mhitimu wa programu hiyo Faraja Michael ameshukuru kwa kupata mafunzo hayo ambapo kwa sasa amejiajiri na kuajiri vijana wenzake.

"Elimu yangu ni ya darasa la tatu lakini hii haikunifanya nishindwe kujiendeleza katika masuala ya ufundi nawashauri vijana wenzangu ambapo wamemaliza Vyuo na hata wale ambao elimu ya yao ni ya darasa la saba, VETA kuna fursa waje wajiunge kupata ujuzi," amesema mhitimu huyo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI