WANANCHI WAPATIWA ELIMU KUJIKINGANA NA MAAFA NANE NANE


Na Asha Mwakyonde,Mbeya 

IDARA ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Wazari Mkuu, Sera Bunge na Uratibu imesema kuwa uwepo wao  katika maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa kwenye viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula', lengo kuu ni kutoa elimu kuhusu madhara na namna ya kuzuia majanga.

Akizingumza jijini Mbeya leo Agosti 3,2023 katika maonesho hayo wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea banda hilo, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara hiyo Charles Msangi amesema wanatoa elimu hiyo ili kuhakikisha taasisi zote, zikiwamo wizara, Idara na wadau wa sekta binafisi wanajua majukumu yao kwa sheria namba 6 ya mwaka 2022 na ushiriki wao katika muundo wa utaratibu na usimamizi wa maafa kuanzia ngazi ya Taifa.

Msangi amefafanua kuwa kuanzia ngazi hiyo wanakamati za ulinzi wa Taifa wa Usimamizi wa maafa ngazi ya Mkoa, wilaya hadi kijiji hivyo lengo lao kubwa ni kutoa elimu kuhusu mfumo na muundo ambao unashughulika na shughuli za usimamizi wa maafa ambazo zimejikita kwa hatua zote kuanzia hatua za awali za kuzuia na kupunguza madhara ya majanga.

Ameongeza kuwa kuna majanga mengine ambayo yanasababishwa na shughuli za kibinadamu kwa kiasi kikubwa wanaweza kuyazuia yasiyokee na kuleta madhara baadae.


"Tumekuja kwa ajili ya kutoa elimu kwa Umma hasa kuhusu sheria ya Usimamizi wa maafa namba 6 ya mwaka 2022 na kanuni zake  na kuelezea kuhusu mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa maafa pamoja na miongozo, mipango ambayo inaelezea shughuli za usimamizi wa maafa kwa kushirikisha wadau," amesema na kuongeza.

"Tunajua yapo majanga ya aina mbili, kuna majanga ambayo yanasababishwa na shughuli za asili kama tetemeko, mafuriko ambayo kimsingi majanga haya hatuwezi kuyazuia lakini katika hatua zetu tunazozifanya za maendeleo kuna hatua zinaweza kufanyika kwa ajili ya kupunguza madhara au athari zake," amesema Mkurugenzi huyo.

Amesema ushiriki wa Ofisi hiyo ni kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu majanga hayo na namna ya hatua za kuzichukua kwa mujibu sera, sheria na taratibu.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wameweka mpango wa kutoa elimu kwa mtu mmoja mmoja kwa kuwa suala la usimamizi wa maafa linaanza na mtu binafisi.

Ameeleza kuwa kuna majanga mengine kama ukame,tetemeko la ardhi ambapo wametoa maelezo ya hatua za kawaida za mfumo wa maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Msangi amesema katika banda hilo wanawataalamu  ambao wanawaelezea wananchi wanaofika bandani hapo pamoja na kuwapatia vipeperushi ambavyo vinalugha nyepesi kuhusu majanga hayo.


"Wataalam wetu wanakuwa wanawapa maelezo namna bora zaidi ya kushiriki shughuli za kupunguza, kuzuia majanga yasilete madhara katika jamii na ushiriki wao pindi majanga hayo yanapaotokea," amesema.

Amesema wanaelewa matukutio yanapotokea wananchi ndio wanaokuwepo katika maeneo hayo hivyo wanawajibu wa msingi wa kwanza kusaidia wale ambao wameathirika wakati wakisubiri vyombo vya serikali kufika katika eneo husika.

Mkurugenzi huyo amesema katika banda hilo wanawataalamu wa kutoa elimu hiyo na  wamepokea wananchi wengi na kwamba hakuna muda waliokaa bila kuhudumia wananchi. 

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA