NMB YAWAPATIA WAKULIMA MIKOPO YA TRILIONI 1.61


Na Asha Mwakyonde, Mbeya 

BENKI ya NMB imetoa mikopo katika sekta  ya kilimo yenye thamani ya zaidi shilingi Trilioni 1.61 kwa ajili ya  wakulima kwa kipindi cha  miaka sita sasa.

NMB ni moja ya ya wadhamini wa  maonesho hayo ya Nane Nane 2023 kwa kutoa udhamini wa shilingi milioni 80 na kufikia  udhamini huo wa shilingi milioni 255 katika kipindi cha miaka minne ya maonesho hayo.

Hayo yamesemwa leo 3, 2023 jijini Mbeya na Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu Straton Njau kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane), ambayo yanafanyika Kitaifa mkoani hapa katika viwanja vya John Mwakangale yenye kaulimbiu isemayo 'Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula',wakati Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa alipotembelea banda la benki hiyo.

Meneja huyo amesema NMB ndio benki ya kwanza nchini kwa  kushusha riba ya  mikopo ya kilimo, uvuvi na ufugaji hadi kufikia asilimia 9, ambapo inatoa mikopo hiyo Sh . 200,000 hadi Sh. bilioni 1 kwa mtu mmoja mmoja, vikundi, taasisi, mashirika na Vyama vya Ushirika vya Wakulima (AMCOS).


"Katika kipindi cha miaka  miwili hii, NMB tumetenga Sh. bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa maghala ya mazao vijijini  lengo likiwa ni  kukabiliana na upotevu na uharibifu wa mazao," ameeleza Njau.

Ameongeza kuwa benki hiyo  tayari imeshatoa zaidi ya Sh. bilioni 7 kati ya hizo zimeshakopeshwa  kwa wakulima hao ndani ya mwaka huu pekee. 

Akizungumzia programu inayoendeshwa na serikali ya Kuandaa Vijana na Wanawake kwa Kesho Iliyo Bora (BBT), amesema wametenga Sh. bilioni 20 kuwezesha Program hiyo kwamba mchakato wa kukamilisha hilo unaendelea baina yao na Wizara ya Kilimo.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA