Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na Maafisa Ustawi wa Jamii wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa Maafisa hao uliofanyika Septemba 06-07, 2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekhalaghe akieleza umuhimu wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutumika kwa maendeleo ya jamii wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii uliofanyika Septemba 06-07, 2023 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (Afya) Dk.Wilson Charles akielezea namna Ofisi hiyo unavyoratibu utekelezaji wa Afua mbalimbali za Ustawi wa Jamii katika Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii uliofanyika Septemba 06-07, 2023 jijini Dodoma.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Dkt Nandera Mhando akifafanua masuala mbalimbali ya Idara hiyo katika kusimamia utekelezaji wa Afua mbalimbali za Ustawi wa Jamii wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Ustawi wa Jamii uliofanyika kuanzia September 06-07, 2023 jijini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa, Halmashauri na Taasisi mbalimbali wakifuatilia shughuli ya kufunga Mkutano wa Mwaka wa Maafisa hao uliofanyika Septemba 06-07, 2023 jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
SERIKALI itaendelea kuboresha huduma na mazingira wezeshi kwa Maafisa Ustawi wa Jamii ili waendelee kufanya kazi kwa uweledi kuisaidia jamii.
Hayo yameelezwa leo Septemba 7,2023 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis wakati akifunga Mkutano wa siku mbili wa mwaka wa Maafisa Ustawi Jamii, ameeleza kuwa mkutano huo umelenga kujadili mikakati itakayowezesha ufanyaji kazi mzuri kwa maaflsa hao.
Amesema Maafisa hao wanafanya kazi kubwa ya kukonga nyoyo za wanajamii pale wanaposimamia majukumu yao ipasavyo kwa kuhakikisha jamii inapata huduma inayostahili.
"Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anajua matatizo ya jamii ndio maaana ameunda Wizara hii," ameeleza Naibu Waziri Mwanaidi.
Awali Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk. Seif Shekhalaghe amebainisha kuwa huduma zinazotolewa na maafisa hao ni muhimu kwa mstakabali wa Taifa lenye amani.
"Itapendeza mkutano huu mkija na maadhimio wizara yetu itatekeleza, tunathamini michango yenu," ameeleza Dk. Shekhalaghe.
Aidha amewaomba watendaji waliopo wizarani kusikiliza kero za Maafisa hao pindi wanapoziwasilisha kwao.
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),(Afya) Dk. Wilson Charles amesema wanatambua upungufu wa rasilimali huku akiwasisitiza maaflsa hao kufanya kazi kwa bidii.
"Endeleeni kupambana kazi mnayoifanya kwa kushirikiana na wadau ni nzuri, hii ni vita kwa sababu wazazi wanaungana kushirikiana na wahalifu wa vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watoto," amesema.
Ameongeza kuwa ataendelea kusimamia wizara hiyo kwa kutumia miongozo iliyopo.
0 Comments