WANANCHI BUMBWINI WAFUNGUKA MAZITO MBELE YA RC AYUB, ATATUA KERO ZAO KWA VITENDO

Na Andrew Chale, Kusini Unguja, Zanzibar.

WANANCHI wa Bumbwini wa Shehia tatu za Misufini, Mangapwani na Kidazini wamefunguka mazito mbele ya mkutano wa wazi wa Wananchi kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,  Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud huku baadhi ya kero hizo akizitatua papo kwa papo.

Katika mkutano huo wa ziara yake ya siku ya kwanza jana mchana, Septemba 4, 2023 iliyofanyika kwenye uwanja wa Vidimni, Mhe RC Ayoub ameweza kupokea kero mbalimbali za Wananchi huku kero kubwa ikiwemo ukosefu wa maji, Umeme sambamba na suala la malalamiko ya watu kutolipwa fidia katika maeneo ambayo miradi ya Kiserikali iliopita maeneo yao huku suala kubwa wananchi hao wakilalamikia moja ya Mgahawa wa mwekezaji wa ndani uliopo kwenye fukwe  Shehia ya Mwangapwani kujihusisha na vitendo vya uvunjivu wa maadili wakitaka ufungwe.

Ambapo katika kutatua kero hizo, RC Ayoub ameweza kuwapigia Wakuu wa Idara pamoja na Watendaji wakuu wa mamlaka husika zikiwemo Maji, Umeme na wengine wengi ambao waliweza kujibu moja kwa moja kero hizo ambazo zingine waliahidi kuzifanyia kazi kwa haraka.

Naye Bi. Salma Thabit Abdalah amesema kuwa wamefuatilia suala la Umeme kwa muda mrefu lakini wamekosq majibu hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa kutatua kero hiyo ili waweze kupata umeme sambamba na maji katika maeno yao.

Kwa upande wake, Khamis Athuman,  kero yake kubwa shamba lake la mihogo kutolipwa fidia,ambalo ulipita mradi wa Serikali. 

"Wakazi bwimbwini' wataka Beach Kidimbwi ifungwee

"Viongozi Zanzibar wanafirigisa mambo kuonekana Rais hafai. Tumsaidie Rais kwa kuja kuchukua kero za huku chini,  tunakupongeza Mkuu wa mkoa  kwa kuja huku chini kutusikiliza" amesema Mwananchi huyo kufuatia mkutano huo

Hata hivyo akijibu baadhi ya kero, RC Ayoub amesema.

"Ipo tabia kwa baadhi ya watumishi wa sekta, kufanya kazi bila kutoa taarifa popote. Naomba nitoe maelekezo kwa viongozi wote waliopo kwenye maeneo yangu, wananchi kama wamekuja hawana taarifa muwafukuze.

Mtu akija kufanya kazi hizo zozote, kama hakuna taarifa mumfukuze 'Nikiwa kama mimi mkuu wa mkoa ni marufuku, lazima taratibu zifuate."Amesema RC Ayoub 

Akitolea ufafanuzi suala la eneo la mwekezaji wa ndani ambaye amejenga eneo la Bar na kulaza wageni pamoja na kupiga muziki,ambapo wananchi wamelipa eneo hilo kama 'Beach Kidimbwi ' ambapo amesema Serikali haikutoa kibali kufanya Bar ya kuuza vileo eneo hilo, bali Serikali ilitoa kibali 2022, kwa jina la 'Nice One beach resort' ikiwa kibali cha Mgahawa.

"Yanayotokea sasa kupiga muziki Bar, Nice one beach resort, naifunga rasmi.

Tumepata kero nyingi kwa wananchi vikao vya ndani na mkutano wa wazi, Kuuza madawa ya kulevya kama Unga, vilevi, biashara ya ukahaba mambo mengine huku ni kuvunja maadili, naenda kuufunga usiku  jioni hii nikitoka hapa lengo kulinda maadili na kufuata misingi ya kisheria." Amesema RC Ayoub. 

Ziara hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo katika Shehia mbalimbali za Mkoa wa Kaskazini Unguja. 

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI