WANANCHI WAPATIWA MITUNGI YA GESI KWA GHARAMA NAFUU

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WIZARA  ya Nishati kwa kushirikiana na Kampuni ya Lake Gesi imegawa mitungi 13,500 kwa gharama nafuu kwa Wananchi wa Mikoa Dodoma, Arusha, Mwanza, Morogoro na Geita  lengo likiwa ni wananchi hao  waweze kuachana na matumzi ya kuni na Mkaa ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.

Wakizungumza baada yakupokea majiko hayo kwaniaba ya wananchi, baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Dodoma, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma, George Simbachawene, Job Ndugai  ambaye ni Mbunge wa Kongwa Pamoja na Mbunge wa Bahi, Kenneth Nollo wamempongeza Rais  Dk. Samia Suluhu  Hassan kwa hatua hiyo ambayo itachochea matumizi ya gesi Vijijini na kuachana na uharibifu wa Mazingira  kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.


Naye aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa  Kongwa Job Ndugai amesema mitungi hiyo inasaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

"Suala la kuhifadhi mazingira ni la muhimu katika nchi mitungi hii ni moja  kupambana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi," ameeleza Ndugai.

Aidha Ndugai amesema  msisitizo uliopo kwa sasa ni kwa akina mama na kina baba kuhakikisha mitungi ya gesi inatumika  badala ya kuni na mkaa.


Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Lake Gesi, Matina Nkulu amesema wao wamejizatiti katika utoaji wa huduma ya  mitungi ya gesi vijijini ikiwa ni Pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya Gesi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU