HUDUMA ZA MAWASILIANO KIKWAZO KWA WACHIMBAJI WA MADINI YA SIPNEL

Na Mwandishi wetu

SERIKALI imeombwa kupeleka huduma ya mawasiliano ya simu   za kiganjani katika kijiji cha Epanko  Halmashauri ya Mji Mahenge wilaya ya ulanga   Mkoani Morogoro ili kurahisha mawasiliano katika uendeshaji shughuli za  uchimbaji madini ya vito (Spinel) katika kijiji hicho.

Mbali na hilo pia imeombwa  kuboresha  huduma ya upatikanaji wa nishati ya umeme wa uhakika katika maeneo ya migodi hili kuweza kusaidia kutozalisha kwa hasara kama ilivyo sasa.

Akizungumza wa waandishi wa habari wakati walipotembelea mgodi wa Franone Mining and Gems wanaozalisha madini ya Spinel kwa lengo lakupata elimu kuhusu madini hayo Meneja Mgodi Elias Thomas amesema kuwa wamekuwa na changamoto ya mtandao wa simu za mkononi ambapo mtandao unaopatikana ni mmoja tu ambao pia unapatikana kwa shida.

Thomas amesema huduma ya mawasiliano ya simu za kiganjani ni  muhimu hususani maeneo ya migodini kutokana asili ya kazi zao hivyo ni muhimu kwa  Serikali kulipatia  kipaumbele.

Aidha Thomas amesema kupitia uzalishaji wa madini ya Spinel wameweza kurudisha kile wanachokipata kwa jamii kwakujenga nyumba sita kwa wananchi waliokuwa na uhitaji ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya barabara na kujenga vyumba vya madarasa.

Akizungumzia kuhusu kukatika katika kwa umeme hasa katika maeneo ya migodi amesema hali hiyo inachangia kuendesha uzalishaji kwa hasara hata Serikali pia kukosa mapato  ambapo amaiomba Serikali kuhakikisha maeneo yote ya migodi kuwa na umeme wa uhakika. 

"Mgodi umetoa ajira kwa vijana zaidi ya 200 ambao ni wazawa na siyo wazawa  lakini pia tumekuwa tumechangia uchumi wa nchi kwakuwa waaminifu katika ulipaji wa kodi na tunaihaidi Serikali kuendelea kulipa kodi kwa uaminifu pia kuchangia maendeleo ya maeneo yanayotuzunguka ambapo tunachimba aya madini. "amesema Thomas.

Kwa upande wake Semeni Bakari ambae ni mama lishe  katika  mgodi huo ameipongeza Serikali ya muungano wa Tanzania kupitia Rais  wa awamu ya sita DKT. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema uwepo wa mgodi umesaidia kuwepo kwa miundo mbinu mizuri hasa upande wa barabara ambapo kwa sasa zinapitika muda wote.

Amesema anamshukuru pia mkuwekezaji mzawa ndugu Onesimo Mbise kwa kuwekeza katika eneo hilo kwakuwa wameweza kujipatia ajira na wanaendesha maisha yao bila shaka yoyote na wanaendelea kuimarika kiuchumi.

Huku Jesse Mtui ambae ni mfanyakazi wa mgodi huo amesema kupitia mgodi huo ameweza kupata ajira ambayo inamsaidia katika kuendesha maisha yake.

Ameongeza kuwa kwa kukosekana mawasiliano ya simu za kiganjani yeye kama kijana inampa  wakati mgumu kwa kuwa yuko mbali na familia yake hivyo anakosa kuwasiliana nao kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU