WALIOWAHI KUSOMA IRDP WAKUTANA KUBADILISHANA UZOEFU KUELEKEA MAHAFALI YA 37

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WANAFUNZI walisoma,waliwahi kufanya kazi, wanaofanya kazi, wanaoendelea kusoma na wengine waliostaafu katika Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini. Dodoma (IRDP),wamekutana kubadilishana uzoefu ikiwa ni kuelekea katika mahafali ya 37,yatakatofanyika kesho.

Akizungumza leo Novemba 23,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la Kitaaluma la siku moja la IRDP 
Mkurugenzi wa Mipango kutoka Wizara ya fedha na Mipango Moses Dulle kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulika na Huduma za Hazina kutoka Wizara hiyo Jenifa Omolo amesema kuwa tukio hilo ni maalumu kwa ajili ya wale wote ambao walisoma katika
hicho.

Ameongeza kuwa lengo la kongamano hilo ni kubadilishana 
 uzoefu wa huduma ambazo zinatolewa na chuo hicho katika jamii ambayo ni kufundisha kwa maana ya kutoa maarifa na ujuzi kwa watu.

"Huduma ambayo inatolewa na Chuo hiki ni utafiti pamoja na kufanya kazi ya ushauri elekezi," amesema Dulle.


Kwa upande wake  Mkuu wa Chuo hicho  Profesa Hozen Mayaya  ameeleza katika kongamano hili wao kama chuo walijikita zaidi kutoa zawadi kwa watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali chuoni hapo.

Amefafanua kuwa zawadi hizo wamezitoa kwa walimu waliofanya shughuli za tafiti, kufundisha vizuri na katika masuala elekezi pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kuanzia ngazi ya Shahada ya Uzamili na ngazi ya cheti.

Mkuu huyo amesema kuwa katika Chuo hicho kuna Kituo cha Ujasiriamali na Ubunifu (MEI), ambacho kinatoa wanafunzi wabunifu.

Amesema kuwa kongamano hilo ni shamra shamra za kuelekea katika mahafali ya 37  ya chuo hicho ambayo yanatatajiwa kufanyika kesho.

Dorcas Samson ni mwanafunzi ambaye amelelewa katika Kituo cha MEI, kilichopo  chuoni hapo  anayejishughulisha na uongezaji wa thamani kwenye bidhaa za chakula amesema kuwa anatengeneza unga wa lishe pamoja na soya ya chai.


"Kwa Sasa ni mhiitimu wa kituo hiki cha MEI ni Kituo ambacho kimenilea katika masuala ya ubunifu ninaziongezea thamani bidhaa za chakula kama unga wa lishe na soya ya chai," amesema.

Ameongeza kuwa alipofika chuoni hapo aliona fursa iliyonzunguka ndipo akaanza kuzalisha bidhaa hizo ambapo tayari ameshasajili jina la biashara kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Dorca amefafanua kuwa matarajio yake ya baadae ni kuwa mfanyabiashara mkubwa ambaye atatoa ajira kwa vijana wenzake na watu wengine.

Naye mwanafunzi mjasiriamali  wa Shahada ya Maendeleo ya Jamii chuoni hapo Thabita Pando ameeleza kuwa yupo katika Kituo cha MEI anajihusisha na utengenezaji wa bidhaa za ubuyu zikiwamo kutengenezea jamu ya ubuyu kwa ajili ya mkate.

"Nimehitimu Stashahada ya Maendeleo ya Jamii katika Chuo hiki, na kwa sasa nimejiunga kuendelea kusoma Shahada ya Maendeleo ya Jamii huku nikiendelea kutengeneza bidhaa zangu na kuuza," amesema Pando

Pando ameongeza kuwa tayari ana alama ya biashara pamoja na cheti cha usajili wa jina la biashara yake kutoka BRELA.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU