HATIMAYE DARAJA LA KELEMA MAZIWANI KUANZA UJENZI JANUARI 15,2014

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

UJENZI  wa daraja la Kelema Maziwani  lililopo Kata ya Dalai barabara ya Kondoa- Bicha  Dalai unatarajia kuanza rasmi Januari 15,2024 na kukamilika Machi 2025 kwa gharama ya Sh. bilioni 8.

Daraja hilo lilikatika tangu April 4,
2020 kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikishasha ambalo linalounganisha mikoa ya Tanga, Dodooma na Manyara limekuwa ni kikwazo kwa wasafiri na hata wananchi wanaokizunguka kijiji cha Kelema Maziwani kwa kushindwa kupitika zaidi ya miaka mitatu sasa.

Akizungumza jijini Dodoma jana katika kikao cha  Bodi ya barabara ya Mkoa, Mhandisi wa Miradi kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS),Mkoa wa Mhandisi Colman Gaston alisema ujenzi huo unatekelezwa na Mkandarasi  Hari Singh and Sons  kwa gharama ya Shilingi bilioni 8,000,000 na upo katika hatua za awali na maandalizi ( Mobilization Stage ).


Kwa upande wake mbunge wa Chemba Mohamed Moni  alishukuru kuona daraja hilo limetengewa fedha kiasi cha Sh. bilioni 8 na kwamba tayari mkandarasi amepatikana.

" Tunajenga daraja la mita 80 katika daraja ambalo nimekuwa nikiuliza maswali mengi bungeni ni daraja la Kelema Maziwani nichukue nafasi hii kuwashukuru mmezingatia na naamini pengine uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hakutakuwa na maswali mengi ya kujibu," alisema Moni.

Aidha mbunge huyo aliiomba TANROADS kipande cha kilomita 8  kutoka Goima kuunganisha barabara ya Dalai kukiombea bajeti kwa kuwa barabara hiyo ya Dalai itakuwa na lami.

Mbunge huyo aliongeza kuwa itakuwa ni changamoto kiloamita hizo kutoka barabara inapokatia  kwenda Singida kuja katika kijiji cha Kelema Maziwani huku akiiomba TANROADS waingize  katika bajeti kilomita hizo.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma Pili Augustino alisema kuwa jukumu lao kama chama ni kuwasukuma watendaji watekeleze miradi ya maendeleo kwa wakati ili mwakani wanapoingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa wasipate shida kuomba kura kwa wananchi.

"'watendaji mkasimamie madaraja yajengwe kwa wakati, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi chini ya uongozi wake," alisema Katibu huyo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI