KATAMBI: BILIONI 4.26 ZIMETUMIKA KUNUNUA VIFAA KWA WANAFUNZI WENYE MAHATAJI


Na  Asha Mwakyonde, Dodoma

SERIKALI imetoa kiasi cha  Sh. bilioni 4.26 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa vya ufikivu kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum na vifaa husika vimesha nunuliwa na kusambazwa katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji Maalum.

Pia Serikali inaendelea na ujenzi wa Vyuo vipya vinne vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vya Songwe, Mwanza, Kigoma na Ruvuma  ambapo kiasi cha Tsh bilioni 3.4 kimetumika na kwa mwaka wafedha 2023-24 kiasi cha Sh  bilion 3 kimetengwa kwa ajili kuendeleza ujenzi kwa Vyuo husika. 

Akizungumza jijini Dodoma leo Disemba 14,2023 kuhusu baadhi ya shughuli zinazotekelezwa na zinazoendelea kutekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu (OWM-KVAU),Patrobas  Katambi alisema kuwa serikali imetengeneza na kuzindua Mfumo wa Taarifa za watu wenye Ulemavu (PD-MIS), utakao weza kusaidia upatikanaji wa taarifa za Watu wenye Ulemavu na kurahisisha utoaji huduma kwa Kundi hili muhimu hapa nchini.


Ameonggeza kuwa serikali ilitoa kiasi cha millioni 960 kwa ajili ya Ujenzi wa mabweni katika shule zenye Watoto wenye mahitaji maalum nchini na kwamba imetoa fedha kiasi cha sh. milioni 62  kwa ajili ya ununuzi wa maligafi za utengenezaji wa mafuta ya Ngozi ya Watu wenye Ualbino kwa kiwanda cha KCMC ilikuwezesha upatikanaji wa mafuta kwa Watu wenye Ualbino.

Naibu  Waziri huyo amesema serikali imetoa kiasi cha Tsh bilionI 3.46  kwa ajili ya ukarabati Vyuo vya Ufundi stadi na marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu vilivypo Saba Saba -Singida, Yombo -Dar es Salaam, Mtapika -Masasi na Luanzari- Tabora  

Amefafanua kuwa Serikali imeendelea kutoa mafunzo kupitia vyuo 6 vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu ambavyo ni Sabasaba – Singida, Yombo Dar es Salaam, Luanzari – Tabora, Masiwani – Tanga, Mtapika - Masasi na Mirongo – Mwanza vyenye vijana wenye ulemavu wapatao 774 na kiasi cha Tsh 568 Milion kimetumika kuwezesha mafunzo husika.


Naibu Waziri huyo alieleza kuwa 
serikali imeendele kusimamia maadhimisho ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu nchini yakiwemo maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu  Disemba 3, 2023, Wiki ya Viziwi ambayo yalifanyika mwisho mwa mwezi Septemba.

"Siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe ambayo ilifanyika Septemba 30 mwaka huu na Siku ya Watu wenye Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi Oktoba 25,2023," amesema Naibu Waziri Katambi.

Amefafanua kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa wa haki na ustawi wa Watu wenye Ulemavu katika jamii; kutambua shughuli na vipaji vya Watu wenye Ulemavu na kuimarisha umoja na mshikamano.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU