Na Asha Mwakyonde,Dodoma
WATOTO hasa walioaacha shule na wale waliotelekezwa mitaani wengi wanaotumika katika usafirishaji wa dawa za kulevya nchini na maeneo mbalimbali.
Pia jamii imetakiwa kuhakikisha ina wanalinda watoto ili wasishiriki katika biashara ya dawa za kulevya na kuepuka kutumiwa katika kubeba dawa hizo.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma jana Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini wakati akizungumza na waandishi wa habari alisemai wapo kati oparesheni mbalimbali wamebaini kundi hilo la watoto ndio linatumiwa kwenye biashara hiyo.
Alisema kuwa watoto hao wanatumiwa katika biashara hiyo si rahisi kuwabaini na kwamba kupatia oparesheni wanazozifanya waliwabainia ambapo kwa sasa wanashirikiana na jeshi la polisi.
Kamishna jenerali huyo aliongeza kuwa kwa sasa wanatoa elimu Mijini,Mitaani,Vijijini na Familia kwa Familia ili kuhakikisha Wazazi wanawalea watoto wao na kutambua tabia zao mapema ili wasishiriki katika madawa ya kulevya.
"Tunaendelea kubaini mitandao ya dawa za kulevya za Heroin,Cocain na Methadone pamoja na wale wakulima wakubwa wa mashamba ya bangi na mirungi," alieleza.
Kwaupande wake Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Verediana Mlimba alisema kuwa wao kama jeshi la polisi wameweka mikakata mbalimbali ambayo kwa kiwango kikubwa jamii inawasaidia ni pamoja na mradi wa usalama wetu kwanza ambao umelenga zaidi watoto ambao wapo mashuleni kwanzia shule ya msingi,sekondari na vyuoni.
Alisema lengo ni kudhibiti utoro kwani wamegundua kuwa utoro ni zao la uharifu kwani wanaojificha kwenye makorongo maeneo mbalimbali wanatekwa na vijana nakufanyiwa vitu vya kiuharifu ikiwemo kuvutishwa bangi ,kubebeshwa ama kulawitiwa.
0 Comments