TARIMBA AIHOJI SERIKALI JUU YA BIMA YA AFYA KWA WATOTO

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

MBUNGE wa Kinondoni Tarimba Abbas ameihoji  serikali Je, nini kauli ya yake juu ya Bima ya Afya kwa Watoto ni katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Akijibu swali la hilo  leo Januari 2, bungeni Naibu Waziri wa  Afya  Dk. Godwin Mollel amesema kauli ya Serikali kuhusu Bima ya Afya kwa Watoto ni kuwaomba Watanzania wote, Viongozi wote, Kisiasa, Kidini na Kimila kuwa 
suluhu pekee ni wao wote kuungana na Serikali katika kuhamasisha Umma kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pale mchakato utakapoanza. 

Aidha mbunge huyo ameuliza maswali mawili ya ngongeza ambapo  alisema kuwa wanafahamu Taifa  limekuwa na haja ya kuhakikisha wanajenga Taifa  la kesho na kwamba katika kufanya Taifa hilo maana yake watoto wao wawe na afya Bora kutokana na uwepo wa mfumo mzuri.

Ameihoji serikali haioni umuhimu wa kuwa na mfumo ambao utasaidia watoto kuendelea kutunzwa afya zao badala ya kukaa na kusubiri hadi bima ya afya kwa wote iweze kufanya kazi?

Katika swali lake la pili amehoji kwa kutokuwa na mfumo sahihi wa watoto na afya zao  "hatuoni kwamba tunafifilisha, tunapunguza ari ya Taifa hili kuwajenga vizuri watoto kwa minajiliya kuwa na Taifa bora la kesho?

Akijibu maswali hayo Dk. Mollel amesema kuwa mifumo mizuri ndio maana juzi Rais Rais Dk. Samia alienda katika Hospitali ya Binjamini Mkapa (BMH), na kwamba watoto masikini ambao wasingeweza kulipa zaidi ya milioni 50 zilizohitajika kwa ajili ya ya kutibu watoto wenye ugonjwa wa Selimundu (Sickle cell) ambapo wametibiwa Bure na kupona.

" Na mwaka huu  watoto zaidi ya 20 Rais Dk Samia ametoa fedha watatibiwa na kurudi kwenye familia zao," amesema Dk. Mollel.

Ameongeza  katika nchi hii kuna watoto milioni 31 ambapo milioni 1.5 wapo kwenye mfumo wa bima wa sasa na milioni 30.7 wapo katika mifumo mingine iliyopo nchini huku akieleza kuwa kuna mifumo haikosi changamoto na kwamba wanaendelea kukabiliana nayo.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU